Swahili hub |
Afisa mipango wa halmashauri ya Chamwino, mkoani Dodoma, bwana Fred Kaombwe (34) amejiua kwa kujifyatulia risasi mwenyewe kutokana na wivu wa kimapenzi juu ya mke wake.
Imedaiwa kuwa Afisa huyo amejilipua baada ya kumkuta mke wake Vicky Kaombwe akiwa na mwanaume mwingine baa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Bi. Elizabeth Masiaga alisema kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana kwenye majira ya saa 3 usiku huko mtaa wa Madole eneo la Kigamboni.
Taarifa hiyo ilisema marehemu alifariki dunia baadae wakati akikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu kuokoa uhai wake
Marehemu aliweza kumjeruhi mke wake maeneo ya mbavu kwa kuwa alimminia risasi maeneo hayo lakini risasi haikuweza kubaki mwilini
Alisema awali marehemu walikuwa na ugomvi kati yao wa kimapenzi na siku ya tukio mashuhuda waliyoweza kuiambia polisi walisema marehemu alimkuta mkewe akiwa na mwanaume katika moja ya baa eneo hilo
Baada ya kumkuta mwanamke alikimbilia katika gari lake alilopaki pembezoni mwa baa hiyo na kuondoka kukimbia kwa ndugu zake na mume huyo kudaiwa kumfukuzia
Ndipo marehemu alimpiga risasi mkewe wakati akishuka kwenye gari na kufahamu kuwa amekufa na kisha yeye kurudi ndani ya gari na kujipiga risasi ya kifua na kufariki dunia papohapo.
0 comments:
Post a Comment