Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

Showing posts with label Kiswahili. Show all posts
Showing posts with label Kiswahili. Show all posts

Tuvuti ya http://www.swahilihub.com ina Manufaa Mengi

Julius Nyerere, President of Tanzania, during ...
Julius Nyerere, President of Tanzania, during a meeting with US president Jimmy Carter, August 4th, 1977. (Photo credit: Wikipedia)

Mradi mkubwa kuunganisha wazungumzaji wa Kiswahili Afrika Mashariki umeanzishwa na magazeti ya Mwananchi na Taifa Leo, Kenya.

Mbinu za Lugha ya Kiswahili


Mbinu za Lugha
Katika fasihi, mwandishi au msimulizi anaweza kupitisha ujumbe wake kwa njia mbali mbali zinazomwezesha kuwasilisha ujumbe wake vizuri na kwa lugha inayopendeza. Kuna tanzu mbili za mbinu anazotumia mwandishi/msimulizi wa fasihi:
a) Mbinu/Fani za Lugha 
b) Mbinu za sanaa
Mbinu za lugha hutambulikana moja kwa moja kutokana na uteuzi wa maneno yaliyotumika. Msomaji hahitaji kusoma kifungu kizima ndipo mbinu hiyo ijitokeze.
Mbinu za sanaa humhitaji msomaji asome kifungu kizima, au hadithi yote ndipo mbinu iliyotumika ijitokeze.
{Mbinu za Lugha ya Kiswahili}

Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini


UTANGULIZI

Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili na kuiweka katika mizani, upande mmoja ubebe tahakiki zilizozingatia maudhui na mwingine zile zilizoangaza fani, upande wa maudhui utalemewa na uzito na kuanguka. Ni kweli kuwa umuhimu wa fasihi katika jamii unatokana na jinsi ambavyo inaimulika jamii na kuichora kwa madhumuni ya kuihakiki na 

Wanaume msiogope kutahiriwa


WASWAHILI husema kazi ni kazi! Wengine husema kazi nzuri ni ile iliyouwezesha mkono kwenda kinywani. Lakini, kwa bahati mbaya, baadhi ya wanajamii hasa wa siku hizi wamekuwa wakichagua kazi huku wengine zaidi vijana, wakidai kuwa hakuna ajira.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi
Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomoka.

MWANDISHI ADAM SHAFI


MWANDISHI ADAM SHAFI

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…

Shaaban Robert


Maisha
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti. Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.

Lugha ni Njia


UTANGULIZI
Lugha imewahi kufafanuliwa kwa jumla kama mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Wataalamu wengi wa isimu (sayansi ya kuchanganua lugha na kuieleza jamii) kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86 na lugha wanaelekea kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao ( massam ba D.P.B na wenzake 1999, TUKI).

Jifunze Fasihi


Fasihi kama dhana, imeelezwa na wengi kwa kuegemea nadharia na mitizamo
mbali mbali.  Hata hivyo ni muhimu tufahamu ya kwamba maana inayopewa dhana au
kitu fulani, huwa inachukuana na matumizi ya dhana yenyewe, watu wanaohusika,
mahali dhana hiyo inamotokea, na hata kipindi au wakati husika.  Hii ndiyo sababu
twapata maana mbalimbali zikitolewa kuhusu fasihi.  Kwa mfano, waandishi wengi wa
Kimagharibi wamesisitiza kwamba fasihi yahusu tu kazi zilizoandikwa.

Lugha Tukufu ya Kiswahili


Historia ya Kiswahili

Maeneo penye wasemaji wa Kiswahili
Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.
Neno Swahili ni neno la asili ya Kiarabu Sahil lenye maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ (السواحلي) ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani.
Yaliyomo  [ficha]
1 Mwanzo katika miji ya pwani
2 Lugha ya biashara
3 Kiswahili wakati wa ukoloni
4 Kiswahili leo
Lugha ni?

Waandishi Mashuhuri wa Vitabu


Said Ahmed Mohammed



Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe. Hadithi zilizochaguliwa ni Tropical Fish (Samaki wa Nchi za Joto) iliyoandikwa na Doreen Baingana kutoka Uganda, The Madman (Kichaa) iliyoandikwa na Chinua Achebe kutoka Naijeria, na In the Cutting of a Drink (Katika Kutiliwa Kinwaji) iliyoandikwa na Ama Ata Aidoo kutoka Ghana. Hadithi ya Muhammed Said Abdulla” Mke Wangu” ambayo ni hadithi ya zamani sana iliazimwa kutoka katika kitabu fulani cha Rüdder Köpper Verlag ambayo iliwaruhusu kuichapisha katika mkusanyo wetu.

Hadithi




Wosia Wa Babu

Furaha iliyo’je kuwa kwenye kigonda changu  wakati kama huu wa magharibi?. Ha! Ha! Ha!... Siniulize mbona nimekenua ‘ivo, ipo siku katika umri huu wangu, utaijua sababu. Eti watamani kujua sasa ‘ivi?, aha! basi ni hivi, wapo wenye imani kuwa kuishi ni lazima almuradi keshazaliwa. Kubugia chumvi si sheria. Ni kwa kudura zake tu Rabana. Kupata dakika ‘izi za kusema nanyi wajukuu wangu, si kwa umri wangu, si kwa uwezo wangu, si kwa utajiri wala uchochole wangu. Ni majaliwa yake Jalali!.http://visauswahilini.wordpress.com/2012/02/20/kisa-changu/
Pendo la siri.

Makala


Yuko ambaye hajui na hajui kuwa hajui. Huyu ni banadamu ambaye kwake hakuna anachokijua hata kidogo, lakini siyo kwa kosa lake ila bado hajajuzwa juu ya mambo. Kwa jina la karibu twaweza kumwita Mjinga. Ujinga siyo tusi ila tafsiri yake ni mtu yeyote ambaye hafahamu wala hajui chochote. Kwa mfano, wewe kama hujui kitu chochote basi ni mjinga na ukumbuke kuwa ujinga siyo tusi. Lakini pamoja na hayo yote, binadamu wa sampuli hii, huwa hasemi asiyoyajua. Mintaarafu, ukikutana na binadamu wa namna hii ujue kuwa ni mjinga na anahitaji msaada ili kuyajua mambo. Mjinga!!!