Maisha
Shaaban Robert
alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita
10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini
Dar-es-salaam kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti. Akaajiriwa
na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka
1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria
uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia
maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.
Tangu 1944 alihamia
ofisi nyingine ya Hifadhi ya Wanyama, baadaye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mbali na maandio yake
alikuwa na athari kubwa katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili akiwa mjumbe wa
kamati za East Africa Swahili Committee, East Africa Literature Bureau na
Tanganyika Languages Board.
Kwa ujumla Mzee Shaaban
Robert aliandika vitabu ishirini na mbili. Baadhi ya vitabu hivi ni: Adili na
Nduguze, Kusadikika, Kufikirika, Wasifu wa Siti Binti Saad, Baada ya Miaka
Hamsini, na Maisha Yangu. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha za Kichina,
Kiingereza na Kirusi. Alifariki dunia tarere 22 Juni, 1962 na kuzikwa Machui.
Aliacha wake watatu na watoto kumi.
Familia
na Elimu
Wazazi wake wote wawili
walikuwa wa ukoo wa Mganga wa kabila la Kiyao. Hatujui sana habari za wazazi
wake, lakini twajua kwamba jina la baba yake halikuwa Robert. Jina hili ama
latokana na matamshi mabaya ya jina lake hasa au yawezekana kuwa ni jina
alilopewa alipokuwa skuli Msimbazi. Kwa muda mfupi yeye mwenyewe aliandika jina
lake ‘Roberts’, lakini baadaye aliacha kuliandika hivyo. Alizaliwa Vibambani,
ambacho ni kijiji kilicho kusini ya Machui, yapata maili sita kusini ya Tanga,
tarehe mosi January mwaka wa 1909. Hakujiita Myao kabisa, bali alikuwa
mmojawapo wa wachache ambao daima walijiita Waswahili.
Alielemishwa Dar es
Salaam toka mwaka wa 1922 mpaka mwaka wa 1926, akawa mtu wa pili katika
wanafunzi kumi na mmoja waliofaulu mitihani yao na kupewa shahada ya kutoka
chuoni, yaani School Leaving Certificate. Alioa mara tatu: mke wa kwanza
alikuwa Mdigo. Alikuwa na watoto kumi. Alipofariki aliacha watoto watano. Pia
aliacha dada yake (wa baba mmoja) Mwana Saumu, na Mama Yake.
Kazi
Kazi alizofanya
alipokuwa Karani wa Serikali:
Forodhani Pangani na
mahali pengine tokea mwaka 1926 mpaka 1944
Idara ya Wanyama tokea
mwaka 1944 hata 1946
Afisi ya Mkuu wa Jimbo
Tanga tokea mwaka 1946 hata 1952
Afisi ya Kupima Nchi
Tanga tokea mwaka 1952 hata 1960.
Alipandishwa cheo kuwa
Grade III Higher Division mwaka 1929, na katika mwaka wa 1944 akapandishwa tena
kuwa Grade II Local Service Alikuwa mwanachama wa East African Swahili
Committee, East African Literature Bureau, Tanganyika Languages, Tanga Township
Authority.
Kifo na Kumbukumbu
Marehemu akafariki
Tanga tarehe ya 22 Juni, 1962, akazikwa Machui.
Alitunza kwa zawadi ya
waandishi inayoitwa ‘Margaret Wrong Memorial Prize’; pia alikuwa ametunzwa
nishani ya M.B.E.
Vitabu
vyake
Maisha yangu
Kusadikika nchi iliyo
angani
Kufikirika
Adili na nduguze
Masomo yenye adili
Utenzi wa Vita vya
Uhuru
Wasifu wa Siti Binti
Saad
Baada ya Miaka Hamsini
Wengine.
Wengine.
0 comments:
Post a Comment