Wajibu wa dini yoyote ni kuwaongoza binadamu kudumisha maadili fulani mema ili
iwezekane kuishi maisha ya amani na kudumisha hadhi ya binadamu. Ama sivyo itakuwa
haiwezekani sisi kama binadamu kudai kuwa ni bora kuliko viumbe wengine, ambao
lengo lao la kuishi ni kupata tu chakula, makazi na ngono, Kama binadamu pia
wanatumia maisha yao kuzikidhi tu hizi haja za msingi, tutakuwa hatuna kitu chochote
cha zaidi cha kututofautisha kama wanadamu. Binadamu wamevuka maisha ya kujitahidi
kudumu tu na wanao uwezo wa kuchukua hatima ya maisha yao mikononi mwao.
Katika Ubudha tunaita hii Dharma. Viumbe wengine wanaoishi hawawezi kuifikia hii
Dharma kwa sababu akili ya binadamu ni ya juu zaidi kuliko viumbe wote
wengine wanaoishi katika mbingu, Ni akili ya binadamu tu ndio inaweza kuielewa
Dharma... Inafaa kukumbuka kwamba binadamu ndio pekee katika viumbe wote
wanaoishi katika mbingu ambao wanaoweza kubuni mfumo mgumu wa dini. Hata
Devas na Brahmas hawana dini yoyote maalum.
Ingawa tunawaabubu deva(watu wanaokufa baada ya kuishi maisha ya thawabu
duniani) na brahmas(wakazi wa brahma loka,yaani ulimwengu wanakoishi watu wote
waliokufa duniani) na kutoa sadaka kwa majina yao, ni lazima tukumbuke
kwamba akili yetu ya kibinadamu ni ya juu kuliko yao. Ndiyo maana deva na
brahmas hawawezi kuwa Budha. Ni binadamu tu ndiye anayeweza kuufikia
ufahamu wa juu kabisa kwa sababu ni yeye pekee ndiye anayeweza kuiendeleza
akili yake kufikia kiwango cha juu kabisa.
Baada ya kupewa hii akili binadamu anajitahidi kuelewa hali halisi ya kuishi
kwake na kuunda kanuni zinazofaa za tabia ambazo zitamfanya atukuke na astahili
heshima, Watu wafikiriaji , wa kale na wa sasa , wametafakari kwa kina sana
kuhusu maswali matatu ya maisha “ Mimi ni nani ?” “ Nafanya nini hapa ?” “
Nahitajika ? “Majibu ya maswali haya yanaweza kutupa msingi wa kuishi maisha
yenye maana.. Tunaiita hii ndiyo misingi ya maisha.
Misingi ya kuwa binadamu ni ipi ? Kulijibu hili swali kwanza inabidi tujiulize
neno ‘ binadamu ‘ mana yake nini, Lugha za Pali na Sanskrit.zinatumia neno ‘
manussa ‘ au ‘ manusya ‘ kumaanisha binadamu, Ni neno lenye maana sana, Pia
neno la kuingereza ‘ man ‘ linatokana na neno la kisanskrit ‘ manu ‘
linalomaanisha ‘ kufikiri ‘ . Binadamu ndio viumbe pekee wanaoweza kuipalilia na kuiendeleza akili kufikia
kikomo chake cha mwisho kabisa. Kiumbe kama huyo anaitwa manussa (
binadamu ) . Neno ‘ man ‘ pia linatokana na neno ‘ mana ‘ linalomaanisha ‘ akili ‘.
kwa hiyo yule mwenye akili ya kufikiri anaitwa mtu. Na akili yake ya juu mtu
anaweza kuziongoza na kuzielekeza hamu zake na anaweza kuyatengeneza maisha
yake anavyochagua.
Wachina wanamwita binadamu ‘ yule ambaye ana moyo ambao uko tayari kutenda
wema.’ Katika moyo wa binadamu lazima kuwepo huruma na kweli .. Kama
mambo haya mawili hayapo basi mtu hawezi kufikirika kwamba ni mtu kweli,
Wanafalsafa wa magharibi wanamwita mtu yule tu ambaye anafikiri kwa kutumia
mantiki.. Binadamu ndio viumbe pekee wenye mantiki katika vitendo vyao.
Viumbe wengine wanategemea hisia tu kuhakikisha uwezo wao wa kumudu
maisha, kustarehe na kujilinda. Akili ikipaliliwa kwa kuacha mawazo maovu na
kuendeleza thawabu nzuri mtu anaweza kuifikia hii shwari ambayo inaleta
kutakasika kwa akili.
HALI YA AKILI YA BINADAMU
Akili ya binadamu inaweza kupenyeza na kuchambua elements au miundo ya
dunia katika mbingu yote. Akili inaundwa na mawazo yasiyodumu ambayo
yanaibuka na kufifia upesi kama umeme. Kuna nishati nyingi sana katika akili.
Hakuna nishati ambayo inaweza kulingana na akili ya binadamu, Akili ndio
mtangulizi wa kila kitu, akili ndio inayoongoza na vitu vyote vinavyo chanzo
chake katika akili.. Budha amesema , ‘ Siifahamu nishati nyingine kubwa kuliko
akili ya binadamu ambayo inaweza kukimbia mbio sana,. Kwa mfano wale ambao
wamesoma sayansi wanaweza kuelewa mara moja umbile la atom. Atom
inabadilika mara milioni chache katika muda wa nukta moja.
Katika saikolojia ya kibudha, tunaambiwa kwamba kila mara akili inapobadilika
mara 17 , mwili unabadilika mara moja tu. Atom na element pia zinafanya kazi
kwa msingi huo huo. Wale ambao wamesoma baolojia wanaweza kuelewa
kwamba chembe chembe za uhai (cells ) na kila kitu katika mwili wetu
kinabadilika baada ya muda. Nguvu yetu ya akili inaibuka na kutoweka upesi
mara elfu moja zaidi kuliko umeme. Hivyo ndivyo ilivyo akili.
Zaidi ya hayo .akili ndio inayosababisha kila kitu kinachotokea duniani .Budha anasema ‘
‘ ‘Akili ndio imesababisha kila kitu , kizuri au kibaya kilichopo katika mbingu
yote’. Hivi tulivyo ni matokeo ya yale tuliyofikiri.
Ni kwa ajili ya taaswira zetu zilizopotoka ndio tunamlaumu mungu, majini na
mashetani kwa matatizo yetu. Watu wengine wanaamini kwamba mateso yetu ya
leo yamesababishwa na dhambi ya asili iliyotendwa na babu yetu wa kwanza
maelfu ya miaka iliyopita. Kama ni hivyo, mateso ya wanyama yanasabishwa na
nini ? Wao pia wanateseka kutokana na ugonjwa, kuzeeka, na kifo. Nao pia
wanateseka kwa ajili ya dhambi ya asili ? Mimea pia inateseka kutokana na kuugua, kuzeeka na kufa. Nayo pia inapata matatizo haya kwa ajili ya dhambi yao
ya asili ?
Hakuna mtu anayeweweza kuimiliki akili ya mwingine, lakini kama mtu
akiiendeleza akili yake mwenyewe, basi anaweza kuwa na taathira kubwa sana,
kwa wema na hata pia kwa ubaya, kwa akili ya mwingine. Maendeleo ya elimu ya
sayansi yanaweza kutumika vizuri au vibaya na watu kwa sababu zao za ubinafsi.
Kwa upande mwingine, akili inaweza kumilikiwa na kutumika kuitathmini na
kuielewa Dharma na jinsi mbingu inavyofanya kazi.
Kwa kuiendeleza akili watu, kwa mfano, wamegundua nguvu iliyopo ndani ya
atom na wameitumia elimu hii kufanya kazi nyingi zenye manufaa. Kinyume
chake, katika huu utafiti wa atom pia wamevumbua silaha za nyuklia ambazo
zinaweza kuiangamiza dunia yote. Kama akili isipomilikiwa na kuzoezwa kwa
usahihi, hatari zinazoweza kufuatia zitakuwa hazitaswiriki, Mfano mmoja unaokuja
akilini haraka ni jinsi Hitler alivyotumia akili zake nyingi kwa nia za uovu.
Karibu aina zote nyingine za viumbe zinatoweka polepole kutokana na hamu za
kibinafsi za binadamu kunakosababishwa na akili ambazo hazijazoezwa kwa
usahihi. Wanachafua maji na hewa na kuharibu mazingara huku wakidai
wanayaendeleza, kumbe ukweli ni kwamba wanalenga kuleta uharibifu tu. Lazima
tukubali kwamba viumbe wengine hawaharibu kitu chochote katika mazingara kwa
kiwango kile kile ambacho binadamu wanafanya.
HALI TATU ZA MAISHA YA BINADAMU
Kama binadamu tunazo hali tatu. au tabia tatu ,yaani hali ya unyama ,hali ya
binadamu na hali ya utakatifu ..Siyo lazima tusubiri kuzaliwa mbinguni au motoni
ili kuishi mojawapo ya hali hizi .Wanyama wanao uwezo mdogo wa kufikiri
lakini kwa kutumia akili yetu ,binadamu tunaweza kuzithibiti au kuzimiliki tabia
zetu za kinyama na kwa kufanya hivyo tunaiendeleza tabia yetu ya kibinadamu na
tunaweza pia kugundua tabia ya kiroho ndani mwetu
.
Wanyama hawana njia za kuzimiliki tabia zao za kinyama kwa sababu
wanatawaliwa zaidi na hisia tu .Lakini tukiwa kama binadamu ,kwa kutumia akili
zetu kuchambua na kufikiri ,tumeelewa mambo mengine ni sawa na mambo
mengine siyo sawa ,kwamba mambo mengine ni ya kidhalimu na ni ya hatari ,na
kwamba mambo mengine ni mazuri na yenye faida si kwetu sisi tu, bali hata kwa
wengine pia . Hii ndiyo maana binadamu wamewekwa kwenye ngazi ya juu zaidi
kuliko viumbe wengine .
Kwa kuithibiti tabia yetu ya kinyama ,kwa kuacha unyang’anyi au uporaji,na kwa
kuendeleza urafiki na huruma ,tunaendeleza subira ,uvumilivu ,maelewano, umoja
na ushirikiano na nia njema .Hizi ni tabia za kiutu . Lengo la msingi la dini ni kuzihimiza na kuzikuza hizi tabia .Lakini , lazima
tuelewe kwamba baadhi ya hizi tabia zimo ndani mwetu .Tulikuwa tumeziendeleza
baadhi ya hizi tabia njema hata kabla ya dini kutokea . .Akili ya binadamu
imeendelea sana kiasi kwamba inaweza kwa urahisi kuzoezwa ili kufurahia
starehe za mbinguni .Viumbe wengine hawawezi kufanya hivi ? . Akili ya
binadamu imetengenezwa kwa ustadi sana . Inaweza kuunda maisha mabaya ya
motoni. Tofauti na viumbe wengine ambao wanaua kwa kujikinga au kwa kupata
chakula, akili inaweza kumfanya mtu aue kwa tamaa, kwa husuda au hata kwa
kujifurahisha tu. Na bado hatosheki mara tu anapotimiza haja moja, hapo hapo
anakuwa na uchu wa kupata kitu kingine , matokeo yake anakuwa kila wakati
hana furaha.
Mahatma Gandhi amesema, ‘ Dunia inatosha kwa mahitaji ya kila mtu, lakini
haitoshi kwa tamaa ya mtu mmoja tu.’ Binadamu wanapigana wenyewe kwa ajili
ya ule uchu wa ajabu wa kutaka kuwa na cheo zaidi, mamlaka zaidi , pamoja na
anasa zaidi.
AINA NNE ZA DINI
Zipo aina nne za dini katika dunia hii, nazo ni dini ya asili, ya oganaizesheni, ya
ufunuo, na dini iliyowekwa katika mfumo wa maisha.
1. DINI YA ASILI
Katika siku za zamani, zama za zama, binadamu aliishi kwa woga kwa sababu
alikuwa amezungukwa na mambo ambayo alishindwa kuyaelewa. Kwa hiyo akawa
anayaogopa yale mambo ambayo alishindwa kuyaelewa. Woga unawafika wale
ambao wanashindwa kuzielewa sheria za maumbile. Vitu vinavyotisha ni hali tu
za akili; yule mtu wa kale aliposhindwa kuyaelewa maumbile na ukweli kuhusu
matukio katika mazingara yake, akaanza kuamini kwamba kuna nguvu ya uchawi
inayosabisha haya mambo aliyokuwa anashindwa kuyaelewa , kama vile mabadiliko
ya hali ya hewa, kupatwa kwa jua, radi, ngurumo, mvua, upinde wa mvua,
volcano, mafuriko, ukame na mambo mengine mengi. Alifikiri kwamba
yanasababishwa kichawi na nguvu fulani, na kwamba alikuwa anahitajika kutoa
sadaka kuondoa hasira zao ili aweze kuishi kwa amani. Kwa hiyo akaanza
kuiabudu na kuomba msaada wao ili aweze kuyamudu maisha na kupata nguvu
dhidi ya wengine. Baada ya muda vitendo na imani hizi vikawa mwanzo wa
tambiko na sala, ndio ikanza tunaichota dini ya asili.
2. DINI ILIYOUNDWA KWA OGANAIZESHENI
Kabla dini hazijaanza, watu walikuwa nayo mawazo ya kibinadamu, lakini ‘ dini ‘
hasa hazikuwepo. Kwa kuziendeleza tabia zilizokuwepo katika nafsi zao za
ubinadamu na thawabu, wakaanza oganaizesheni ya matendo fulani na kufuatana
na jinsi walivyofikiria wakaunda kanuni za tabia kuiongoza jamii waliyokuwa
wanaishi. Nguvu ya aibu na woga (hiri na ottappa ) ndio mambo yaliyowaongoza na kuamua tabia yao kuhusu wenyewe pamoja na wengine na imani
zikaendelezwa na hatimaye zikawa dini.
3 DINI YA UFUNUO
Inatokana na mafundisho yanayoletwa na mungu mkuu kupitia mesenja au nabii
katika mfumo wa amri au kanuni za dini. Wafuasi wanaamini kwa dhati kwamba
mafundisho wanayoyapata ndio msingi wa tabia yao ya kiroho na katika jamii.
4 DINI ILIYOINGIZWA KATIKA MFUMO WA MAISHA
Katika jamii nyingine, binadamu wanaishi maisha ya kidini kwa kuipenyeza dini
katika saikolojia, falsafa, katika vyama vya siasa, katika shule, na katika maadili
yao kwa utaratibu mzuri. Ili kudumisha amani na tabia njema wametunga kanuni
kuzikuza tabia za kiutu,na kuishi kwa amani na kuyatanzua matatizo yao mengi ,na ili
waweze kuziondoa balaa na vurugu zinazotokea katika maisha. Hizi kanuni
zikihalalishwa na kupewa msingi wa kiroho, ndio inasemekana kwamba dini
imeingia katika mfuma wa maisha.
Mtaalamu maarufu wa kibuddha. Bhikkhu Budhadasa anazipanga dini kwa njia
ifuatayo.
• Dini ya nguvu za muijiza na uchawi ambayo msingi ni woga wa wafuasi
wake.
• Dini ya Imani – ambayo tu msingi ni imani na sala .
• Dini ya Karma - msingi ni mtu kujisaidia , kujitegemea
• Dini ya Hekima -msingi wake ni kufikiri kwa uhuru .
* Dini ya Amani - Msingi wake ni kutojidhuru mwenyewe au wengine
• Dini ya upendo _ msingi wake ni kutoa vyote au kila kitu kwa wengine
MAANA YA UBUDHA NA DHARMA
Ubudha lakini haupo katika makundi hayo manne. Kwa sababu ingawa tunalitumia
neno ‘dini’ kuuuita Ubudha tunaona vigumu kuuuita Ubudha ‘ dini ‘ kufuatana na
maana ya hilo neno kama inavyotolewa katika kamusi. Kwa mfano, kamusi ya
oxford inaelezea dini kama “ muundo wa imani na kuabudu, pamoja na binadamu
kutambua kwamba ipo nguvu kubwa kuliko binadamu inayoongoza, na hasa
mungu ambaye anapaswa kutiiwa.” Neno zuri kupita yote ambalo tunaweza
kulitumia kuyaita kwa usahihi mafundisho ya Budha ni ‘Dharma’ Kwa ajili neno
‘dini’ ndilo limezoeleka, kwa hiyo kwa urahisi tunalitumia hilo neno, lakini
‘Dharma’ ndio hasa neno linalofaa zaidi kwa vile lina maana pana zaidi kuliko
neno ‘dini.
Enyi bhikkhu (watawa), Dharma pamoja na kanuni zinazofundishwa na Budha
zinatoa mwangaza mkubwa sana. Hizi kanuni hazifuatwi kisirisiri. Hizi kaninu ni
dhahiri kabisa kama jua au mwezi. Zaidi ya haya , kuhusu Dharma inayofundishwa
na Budha hakuna ‘mkono uliokunjwa wa mwalimu’. Hii ina maana kwamba Budha kama mwalimu hakuweka siri katika mafundisho yake. Na kwa ajili hiyo hakuna
siri au mafumbo katika Ubudha ambazo zinatakiwa kukubalika tu bila swali lolote
na mfuasi, kwa imani tu kama kipofu.
Budha alikuwa akisema mara kwa mara kwamba yeye hana siri katika kufundisha
kwake. Anafundisha mambo yote anayoyafahamu. Ile tabia ya mwalimu kufahamu
jambo, lakini bado halifundishi, anawaachia walimu wengine. Yaani,tabia ambayo
mwalimu hafundishi kila kitu anachokifahamu,kwa sababu yoyote ile, lakini siyo
kwa vile mwalimu hafahamu analotakiwa kufundisha, hii haikuwa tabia ya Budha.
Dharma ndio ukweli wa juu kabisa ambao umefundishwa na Budha. Ni njia
tukufu ya maisha ambayo wakati wote inatusaidia na kutudumisha juu na
haituruhusu tushuke katika hali nyingine za mateso kama vile motoni, au maisha
ya kinyama au maisha ya ahera, kama mashetani au kama viumbe wengine
ambao hawajabahatika. Kwa hiyo kama tukiifuata Dharma, Dharma itatuhifadhi na
kutusaidia kikamilifu, haitaruhusu tuteseke katika hali zozote za mikosi.
Hii ndiyo maana ya neno Dharma katika ubudha. kwa vile ubudha siyo dini ya
ufunuo, Budha hakupata habari zozote kutoka mbinguni kwa sababu hakuwa na
mwalimu yoyote wa kumfundisha kuufikia mwangaza, Alichofanya ni kutumia
juhudi yake yote, kuyaondoa kabisa mawazo maovu, maneno maovu na matendo
maovu, na kwa kupalilia tabia zote njema, kwa kuitakasaa akili yake, hatimaye
alifikia utakaso na umakini wa akili kiasi kwamba alielewa kikamilifu jinsi kila
sehemu ya mbingu inavyofanyo kazi. Hii ndio tunaita kuufikia mwangaza.
Ubudha ni matokeo ya juhudi za mtu mkubwa aliyejitolea maisha yake na muda
wake kutafuta ukweli wa juu. Lazima tueleze tuna maana gani tunaposema ukweli
wa juu . Kwa sababu watu wengi wanadai kwamba wanaufahamu ukweli.,lakini
hakuna mapatano kati yao kuhusu huo ukweli. Wabudha wanamaanisha nini
wanapolitumia neno hili? Tunajua kwamba zipo kweli za aina nyingi. Lakini siyo
zote zinaweza kuitwa ukweli wa juu. Kweli fulani zinaweza kuwa sahihi kwa
kipindi fulani,lakini baadaye, kwa ajili ya mabadiliko katika hali halisi, hazibakii
kuwa kweli. Ukweli ambao umefahamika na kuhubiriwa na Budha ni ukweli wa
juu, kwa sababu hakuna mtu yoyote anayeweza kuupinga usahihi wa neno hata
moja alilozungumza, hata akitumia uchambuzi wa kisayansi. Ni ukweli wa juu
kwa sababu unadumu milele na hauwezi kubadilika kufuatana na muda au hali
yoyote. Imani nyingine nyingi zilizoonekana kwamba ni kweli hapo mwanzo
imebidi zirekebishwe kufuatia maendeleo katika ugunduzi wa sayansi Mafundisho
ya Budha pekee ndio hayajapingwa, na pia yanathibitishwa na ugunduzi mpya wa
sayansi. Maadili aliyoyafundisha Budha kwa msingi wa ukweli wa juu. pia ni
halali ingawa yametokea maendeleo makubwa. katika ustaarabu (civilization).
Wabudha hawana sababu ya kujieleza upya kuhusu mada kama vile
☯ Euthanasia - kumuua mtu anayeishi kwa kutumia mashine
☯ Mercy killing - kuua kwa huruma
☯ Birth control - uzazi wa majira
☯ Pre-marital sex – kujamiiana kabla ya ndoa ☯ Animal rights – haki za wanyama
☯ Environment nk mazingara
KWA NINI DINI INAHITAJIKA
Tukizumgumza kwa ujumla ni lazima tukubali kwamba dini. zote zimeleta faida
fulani, ingawa wasomi wengine kama Bertand Russell wanasema dini imewaletea
binadamu madhara zaidi ya wema. Kuhusu fitina, chuki na ubaguzi kama
zinavyoelezwa na wana dini tofauti anasema ‘ Wale wasiokuwa na dini wanaishi
kwa amani bila kupigana na kubishana. Wale ambao wana dini mara nyingi
wanapigana kwa sababu ya imani zao tofauti za dini ‘ Lakini sio wote
watakubaliana na yeye.
Kila dini kubwa , kama ni Ukristu, Ubudha, Uislamu au Uhindu imewasaidia
sana binadamu. Kama binadamu wameweza kutenda maovu ingawa kuna dini., je
ingekuwa ni maovu gani ambayo yangeweza kutokea kama wangekuwa hawana dini
ya kuiamini. Kama kwa mfano serikali za dunia zikitangaza kwamba sheria
hazitashinikizwa kwa muda wa saa 24, muda huo unaweza kutosha kulianganiza
kabisa taifa. Na kama dini isipokuwepo kuwathibiti binadamu tatizo hilo litakuwa
kubwa zaidi. Kwa hiyo hatuwezi kuilaumu dini kwa tabia ya binadamu.
Lazima tuongeze hapa kwamba wapo watu wastaarabu ambao ni wema katika asili
yao na hawahitaji uthibiti unaoletwa na watu wa dini. Budha alisema kwamba
mafundisho ya dini yanapaswa kuonekana kama raft ya kumsaidia mtu kufika
ng’ambo ya pili. Mtu akifikia kiwango cha juu cha maendeleo ya kiroho, hahitaji
mwongozo tena, anaishi maisha ya kufuata maadili . Wengi wetu tunaihitaji rafti,
misingi ya kidini kutusaidia kuishi kwa maadili na kukamilika kiroho.
MISINGI YA KIDINI NI MUHIMU
Kama binadamu tunao wajibu wa kudumisha misingi fulani mizuri kwa faida yetu na wengine, Hii
inaleta maana nzuri, kwa sababu tunapofuata kanuni, pia tunawalinda wengine. Kama sisi
hatujakamilika, ikiwa tunataka kuishi vyema na jirani , lazima tuhakikishe kuwa tuna uzio , ama sivyo
kutatokea ubishi, vurugu na kutoelewana. Ttukijenga uzio au ukuta, sio tu tunailinda nyumba
yetu na familia yetu, lakini pia tunazilinda nyumba za jirani zetu. Kwa hiyo kufuata kanuni ni
sawa na hivi. Tunapoamua hatutaua au kuwadhuru wengine , basi tunawaruhusu wengine kuishi kwa
amani bila woga. Huu ni wema mkubwa sana tunaowafanyia wengine. Tunapaswa kuacha
kuwatapeli na kuwadhulumu wengine ili waweze kuishi kwa amani bila kutuogopa au kutushuku.
Kama tunafahamu jinsi ya kutimiza wajibu wetu, tunadumisha hadhi yetu ya kibinadamu pamoja
na akili yetu, kwa kufanya hivyo tunadumisha amani, muafaka na shwari katika maisha yetu.
Lakini kama Robert Frost anavyosema katika shain lake zuri ‘ Kutengeneza Ukuta’ kama sisi ni
wema kwa asili, na jirani zetu ni wema kwa asili, basi uzio hazitahitajika. Jamii zingine za kale
ambazo zinaitwa hazijaendelea zilikuwa zikiishi namna hiyo. Lakini sisi, hasa tunapoishi mijini,
tunahitaji uzio za dini kujilinda wenyewe pamoja na kuwalinda wengine.
Ili kufanya hivi tunapaswa kuzifuatwa kanuni za dini (sila) sila ina maana nidhamu ya kuizoeza
akili. Tunajizoeza kwa kuifuata misingi fulani ya dini kwa kuona hatani iliyopo katika kuipuuzia.
Kuna tofauti katika kanuni za kibudha na amri au sheria za kidini za imani nyingine. Watu wengi wanayatii majukumu yao ya kidini kwa kuogopa kuadhibiwa. Inawezekana kabisa bila kutishiwa
kwenda motoni , watu wengi wangezipuuzia sheria zao za kidini.
Ipo njia yenye sehemu mbili ya kufuata wakati wa kuzitii sila au kanuni. Tunapoacha kuua kwa
kuelewa kwamba tutawafanyia ukatili na mateso viumbe wengine, hiyo inaitwa Varitta Sila.
Kuacha kufanya uovu (kuepuka, kujizuia ). Wakati huo huo tukikuza wema, huruma, maelewano,
hiyo inaitwa Caritta Sila. Kutenda wema (matendo ya wema). Hivi vipengele viwili vya thawabu
viendelezwe, vya kujizuia kufanya uovu na kutenda matendo mema.
Isipokuwepo adhabu, watu wataichukua fursa hiyo kutenda matendo maovu bila
kuonyesha huruma yoyote. Katika Ubudha kuzIngatia sila au kanuni kuna maana;
‘Naizoeza akili yangu iache kufanya mambo fulani yenye madhara, siyo kwa ajili
ya mungu au kuogopa adhabu yake, isipokuwa kwa kuelewa kwamba hayo ni
makosa. Siogopi adhabu au kutegemea zawadi, lakini nafanya hivyo kwa vile
ndivyo ninavyotakiwa kufanya, kwa sababu inaleta faida kwa wengine na kwangu.’
Budha amesema; ‘ Nawashauri kutokana na uzoefu wangu. Siyo habari ambazo
nimeshushiwa kutoka juu. Nimefanya matendo mabaya nilipozaliwa karne zilizopita
na nakumbuka jinsi ilivyobidi niteseke kwa ajili ya makosa hayo. Ndio maana
nawaambia ni bora muache kutenda matendo mabaya ili muepushe mateso. Pia
nimefanya matendo mema mengi nilipozaliwa karne zilizopita, na naweza kuelewa
maisha mazuri, ya amani na fanaka niliyoishi kwa ajili ya hayo matendo mazuri.
Kwa hiyo nawashauri ninyi pia mtende matendo mazuri ili mpate matokeo hayo
hayo mazuri. Kama unataka kufahamu zaidi kuhusu hili somo, soma hadithi za
Jataka ambazo zinaelezea kuhusu Budha katika maisha yaliyopita.
Katika Ubudha hatuwezi kukuta amri, dogma, sheria za dini au vitisho vya
adhabu ya kidini. Dini kazi yake siyo kawaadhibu watu ila kuwashauri watu la
kufanya na lile ambalo siyo la kufanya. Ukifanya tendo lolote la kiovu,
utakumbana na matokeo yake. Siyo Budha au dini itakayokuadhibu. Kitendo
chako mwenyewe ndicho kinachokutengenezea mbingu yako au moto. Mwingine
hawezi kufanya hivyo.
Kama nilivyosema mwanzo hata watu wa kale walikuwa na maadili katika nafsi
zao na walikuwa wanaweza kutofautisha kati ya sahihi na siyo sahihi. Lakini
jamii zilivyoendelea hizi hisia za asili ziliendelezwa na kutengenezwa kuwa
kanuni za tabia kudumisha sheria na usalama. Kuhakikisha kwamba hizi zitafuatwa
viongozi wakasema kwamba zimethibitishwa na mungu pamoja na zawadi au
adhabu za milele. Kwa njia hii, tunaweza kusema kwamba dini zimewasaidia
binadamu.
FAIDA YA KUTOSHEKA
Siku moja mfalme fulani alimwendea Budha na kumuuliza swali. ‘ Ninapowatazama
wafuasi wako naona shwari, uchangamfu na ngozi inayong’ara. Pia nimesikia
kwamba wanakula mlo mmoja tu kwa siku, lakini kwa kweli nashindwa kuelewa
wanaweza vipi kuudumisha mwenendo huu wa maisha.’ Budha akampa jibu zuri’ “
Wafuasi wangu hawayajutii matendo waliyoyafanya zamani isipokuwa wanajitahidi zaidi na zaidi kutenda matendo mema. Siyo kwa kujuta, kusali na kuabudu
isipokuwa kwa kuwasaidia wengine ndio watu wanaweza kufanya toba kwa
makosa waliyoyafanya zamani. Wafuasi wangu hawana wasiwasi kuhusu mambo
yatakayowafika baadaye. Wanatosheka na chochote wanachopata na kwa hiyo
wanadumu katika hali ya kutosheka. Hawawezi kamwe kusema hiki au kile
hakiwatoshi. Huo ndio mtindo wa maisha yao kwa hiyo wanaweza kuidumisha
shwari, uchangamfu na kung’ara ngozi kwa ajili ya huko kutosheka.”
Mtu yoyote anaweza kuudumisha huu uchangamfu kwa kutosheka. Kama mtu
akiuliza kwa nini hatuna furaha katika maisha yetu ingawa vitu tulivyo navyo ni
zaidi ya mahitaji yetu, ni njia gani sahihi ya kumjibu ? Jibu sahihi ni, kwa sababu
hatutosheki ,’ Kama tungetosheka, tusingesema kwamba hiki au kile ni pungufu.
Hatuwezi kutosheka kwa ajili kuna upinzani kati ya hamu zetu za kibinafsi
ambazo hazina kikomo na sheria ya kutodumu kwa vitu (anicca )
Moja kati ya ushauri mzuri uliotolewea na Budha kwetu sisi ili tuuzingatie kama
msingi ni “ Kutosheka ndio utajiri mkubwa kuliko yote,’ Mtu tajiri haina maana
kwamba anacho kila kitu, mtu tajiri kila wakati anahofia kuhusu uhai wake. Kila
wakati yupo katika hali ya woga na wasiwasi, akifikiria kwamba watu
wanasububiri kumdhuru au kumdhulumu. Tajiri hawezi kutoka nje bila mlinzi, na
ingawa anayo milango mingi ya chuma na kufuli katika nyumba yake, hawezi
kulala bila woga na mashaka.
Kwa kulinganisha naye, mtu aliyetosheka ni mtu mwenye bahati sana kwa sababu
akili yake imeepushwa na usumbufu wowote wa aina hiyo. Yeye ndiye tajiri
kweli. Kwa hiyo kutosheka ni nini? Wakati mtu anapofikiria ‘Kiasi hiki kinatosha
kwangu mimi na familia yangu, na sihitaji zaidi ya hivi ‘ huko ndiko kutosheka.
Kama kila mtu akifikiria namna hii, basi hayawezi kuwepo matatizo yoyote.
Tukidumisha kutosheka kwa namna hii, husuda haiwezi kuivuruga akili yetu na
kwa hiyo tutawaruhusu watu wengine wastarehe katika maisha yao. Kama hakuna
husuda, hasira pia haiwezi kutokea, kutakuwa hakuna dhuluma na umwagaji damu
na kila mtu kwa hiyo ataishi kwa amani.
Maisha ya kutosheka daima yanampa mtu matumaini na imani Hii siyo ndoto ya
mchana. Kwa karne 25 watawa wa kIbudha wameishi maisha haya ya amani
katika maskani zao. Na walei wengi wa Kibudha pia wameishi maisha ya
kutosheka bila kuruhusu tamaa za kuvuka mahitaji yao ya msingi. Ni ajabu sana
jinsi ambavyo tunahitaji vitu kidogo sana kutosheka. Fikiria kuhusu jambo hili.
JIFUNZE KUKABILIANA NA MATATIZO YA MAISHA
Kwa sababu ya tamaa za kibinafsi, tunataka tuishi maisha ambayo daima
hayabadiliki, ya amani na fanaka bila kujali kwamba vitu vilivyopo mbele yetu
havidumu. Kwa hiyo tamaa zetu za kibinafsi haziwewi kutoshelezwa kwa sababu
kila kitu hakidumu. Mabadiliko ndio kawaida ya mbingu yote. Hakuna kitu
kinabakia vilevile, na tunahukumiwa kuwania vitu ambavyo daima vipo nje ya
ulingo wetu – kwa sababu sisi na hivyo vitu vinabadilika mara tu vinapoguswa.
Lakini bila kujali mabadiliko hayo, tunasukumwa na kuhadaika, na tamaa za
ubinafsi, bado tunawania maisha ambayo hayabadiliki
Siku moja Budha alimshauri Ananda; kama mtu yoyote akiuliza swali kwa nini
kifo kinatokea, itabidi uwaambie kinatokea kwa sababu watu wanazaliwa, kama
hakuna anayezaliwa kutakuwa hakuna kifo. Kama ukitaka kukizuia kifo kwa nguvu,
basi huyajui maumbile Na ukifanya hivyo utakuwa unaenda kinyume na sheria za
maumbile.
Watu kwa ujumla wanapenda uzazi lakini wanaogopa sana kuoza na kufa.
Machweo ya jua katika nchi moja ni mawio ya jua katika nchi nyingine, kwa
jInsi hiyo hiyo, kifo siyo mwisho wa maisha, kwa vile kifo ni mwanzo wa maisha
mengine. Kuzaliwa kiumbe ndio mwanzo wa kifo. Kifo ndio mwanzo wa maisha
Kuzaliwa kunaleta cheti cha kifo kwa hiyo tukitaka kuepusha kifo, inabidi
tuepushe watu kuzaliwa.
Kwa hiyo tunapaswa kuwa na hekima na kuacha kurudia makosa yetu na tujitaya
rishe kwa maisha ambayo yatakuwa hayana mateso.
Tukichunguza kwa makini tunaweza kuelewa kwa nini dunia imejaa dhuluma na
uonevu. Tunaanza kuona kwamba hiyo siyo kazi ya muumbaji kigeugeu bali
inatokana na matendo yetu mema au mabaya ya zamani. (karma ) tunaweza kuona
taathira ya matendo yetu mema au mabaya hata katika maisha haya, ukitenda
mema yanakufika mema, ukitenda mabaya yanakufika mabaya. Hakuna mtu yeyote kati ya wale wanaoishi kwa thawabu haiamini sheria hii ya
karma,kama yeye ni Mbudha au hata kama hana dini. Na wote,isipokuwa wachache tu
,kati ya wale wanaoishi kiovu,hawaamini katika karma.Kwa sababu mambo yao kila
wakati ni ya kufuru.,kwa vile wanasema,”Tule na tunywe kwa sababu kesho
tutakufa”Kuongea namna hii ni ishara ya kuendekeza starehe kupita kiasi.Hizi falsafa za
kula na kunywa kumbe ndiyo chanzo cha misemo ya kuipinga Dharma
UBUDHA KWA WALEI
Maisha ya kidunia yana matatizo sana. Kwa hiyo siyo rahisi kwa walei kuishi
maisha ya dini. Wakijaribu kuishi maisha ya dini kwa kubadilisha tabia zao hii
inaweza kuleta usumbufu kwa watu ambao wanaishi miongoni mwao. Watu wa
familia yao au rafiki watashindwa kuyaelewa haya maisha yao mapya;. Lakini
wakiyabadilisha maisha yao polepole wengine wanaweza kujirekebisha na kwenda
nao sambamba.
Kwa upande mwingine, mtu anaweza kuishi maisha ya dini bila kuwasumbua
wengine kwa kuwa na upole, uaminifu, subira, uvumilivu, umoja, maelewano na
ufahamu. Lakini hata hapo pia, hizi tabia nzuri zinaweza kuleta matatizo iwapo
wengine watataka kukudhuru kwa ajili ya upole wako Siyo lazima uwe na
thawabu kupita kiasi. ili uishi maishi ya dini kwa walei. Jaribu tu kuishi maisha
ya kawaida.
Budha alianzisha hii njia ya kuishi inayofaa kwa walei kwa ajili ya matatizo
waliyo nayo, Walei hawatakiwi kuwaiga watawa. Na watawa hawatakiwi kuwaiga
walei. Leo hii, utaona watawa wengine wanaishi kama walei, na walei wengine
wanaishi kama watawa.
Kwa kutambua ugumu unaowafika katika kutimiza majukumu yao ambayo inabidi
wayatimize ili wazitunze familia zao, watu inawabidi wafanye mambo fulani.
Budha alisema wanaweza kupata furaha ya aina nne;- kwa kuchuma hela na
kuziwekeza(investing), kwa kustarehe kiasi katika anasa za dunia kwa kutumia
fedha ambazo wamezipata kihalali, kwa kuepusha madeni kwa kuhakikisha
kwamba hela zao wanazitumia vizuri, na kwa kuishi maisha ya thawabu ,watu
wakielewa kwamba hawajamfanyia ubaya mtu yoyote ,wanakuwa hawana sababu
ya kujisikia vibaya. Hisia hii ya raha ndio furaha kubwa kuliko zote anazoweza
kuhisi mtu . Furaha zote nyingine zisizokuwa na maana zitatoweka akilini mbele
ya furaha hii .
Hii hali ya furaha ambayo wanaidumisha na kuibakiza katika akili , itabaki nao
mpaka siku ya kufa na itawasaidia kupata maisha mazuri watakapozaliwa tena .
Kwa sababu wataondoka duniani na akili ambayo haijachanganyikiwa . Hivi ndivyo
watu wanavyotakiwa kurekebisha maisha yao ikiwa wanataka kuishi maisha ya
kidunia kwa faida. Tofauti na walei , wapo watu wachache ambao kwa hiari yao
wanaamua kuyaacha kabisa maisha ya kidunia na kuwa watawa . Watu hawa
wanakuwa na amani ya aina tofauti kabisa .
KUWA NA AKLI YA WAZI KATIKA UBUDHA
Upali ,mfuasi tajiri sana wa dini nyingine , wakati fulani alikuja kumuona Budha
na kumwambia kwamba alitaka kuwa mfuasi wake. Budha alimuuliza, “ Kwa nini
unataka kuwa mfuasi wangu? “ Upali akajibu , “Watu wanasema kwamba
mafundisho yako ni mazuri’ Budha halafu akauliza, “Umeshayasikia mafundisho
yangu yoyote ?” Upali aliposema bado ,swali la Budha lililofuatia lilikuwa “ ,Sasa
unajuaje kama utaweza kuyafuata mafundisho yangu au la; Hiyo siyo njia ya mtu
kubadili dini yake ,Mtu ni lazima ajifunze na ajaribu kuyaelewa mafundisho kabla
hajaamini .”
Hapo Upali akawa na dhamira zaidi ya kumfuata Budha na akasema “Muadhama,
nadhani huu ushauri wako unatosha kabisa kwa mimi kuelewa mafundisho yako
yalivyo. Ingekuwa nimemfuata kiongozi wa dini nyingine , angenipokea na
angetangaza kwamba mtu fulani pia amekuwa mfuasi wa dini yake. Lakini badala
yake muhashamu, wewe unanishauri kuisoma na kuamua kama nataka kuyafuata
haya mafundisho.”
Budha alipotaka kuhubiri , hakuhubiri kama vile anataka kutoa hotuba
hadharani.Alichunguza akili na uwezo wa kufahamu wa wasikilizaji wake. Na
aliwashauri kufuatana na uwezo wa akili yao kushika mambo ili waweze
kuyaelewa mafundisho yake kwa urahisi.
JINSI YA KUMUONA BUDHA .
Mmoja wa wafuasi wa Budha aliyekuwa akiitwa Vakkali alikuwa na tabia ya
kumtazama Budha kila siku, kuutazama mwili wake. Budha alipogundua hili
akamwuliza, “ Unafanya nini hapa? Jibu lake Vakkali lilikuwa “
Muadhama , ninapovitazama viungo vyako vilivyo shwari , na ngozi yako
inayong’ara najisikia vizuri sana.” Baada ya hapo Budha akamwuliza, “Unategemea
kupata faida gani kwa kupendezewa na mwili ambao ni mchafu , unanuka , wenye
sura mbaya, na usiodumu? Mtu anayeiona Dharma, anamuona Budha. Hii
inakusaidia kumuelewa Budha wa kweli. Kama unachotaka ni kumuona Budha wa
kweli., basi unapaswa kumuunda Budha huyo katika akili yako kwa kupitia
mafundisho yake.,
Tunayatazama maisha yetu visivyo, Tunaiona miili yetu kama ndio maisha
yenyewe. Hatulitazami hili swala kwa usahihi. Nguvu za akili na maisha yetu
vyote vinafanya kazi pamoja. Mwili ni nyumba tu ya roho zetu. Tunayatumia
maisha yetu yote kuutunza, kuulisha, kuuosha, kuupendezesha mwili wetu, kwa
kutumia hela nyingi, bila kuelewa kwamba miili yetu inaleta matatizo mengi na
mateso.
MISINGI MITATU MUHIMU KATIKA UBUDHANidhamu [sila],kuiendeleza akili [samadhi],na kupata hekima, ndio misingi mitatu
ya maisha ya binadamu. Binadamu tu ndio wanaweza kuziendeleza hizi tabia
nzuri. Lengo kubwa katika hii misingi mitatu ya Ubudha ni kuzifuata kanuni
[sila].
SILA.
Mtu ni kiumbe ambaye anaishi katika jamii na anaendeleza tabia yake kwa
kuhusiana na jamii anayoishi, kwa hiyo kila analolifanya linaleta taathira sio tu
kwake lakini pia katika jamii yake. Kuzingatia maadili pia kutaleta taathira.
Maadili yanajumuisha thawabu zote za watu wa heshima. Inalinganishwa na
thawabu kwa ujumla, na mambo mengi yanayostahili sifa yametafsiriwa kuhusiana
na malengo ya kujitakasa na kujizuia , katika matendo, maneno na mawazo ya
mtu. Kwa kawaida sila inaeleweka kumaanisha kanuni tano za maadili ambazo ndizo
sheria za mlei. Wanatakiwa kuanza safari yao ya kiroho kwa kuzifuata hizi kanuni
tano, na kila mlei anategemewa kuzifuata hizi kanuni za msingi.
Na pia kufuatana na mwenendo wa Ubuddha hizi lazima zifuatwe kwa kuzingatia uzoefu
na mantiki. Lengo la mwisho la Ubuddha linavuka dhana hii,lakini wakati wote mtu
lazima aishi kwa uhusiano na mambo ya dunia hii, na kwa kuzifuata kanuni hizi tano,
Wabudha wanaishi kwa kuzingatia hali halisi ya dunia hii .Binadamu amegundua kwa
kutumia utashi wake pamoja na manitiki kwamba akiifuata njia fulani,anaweza kufaidika
yeye pamoja na dunia nzima.Kwa hiyo anatumia utashi wake kuifuata hiyo njia. Huku
ndiko kuutambua ubinadamu wa mtu kutambua uwezo wake na wajibu.
Sila au maadili maana yake ni kwamba lazima tujifunze kuishi kama watu ambao
hawaleti madhara,watu wapole. Tunatakiwa kuishi bila kuivuruga amani na furaha ya
wengine.Tukiweza kufanya hivi itakuwa mafanikio makubwa sana. Nidhamu,tabia
njema,kanuni na maadili yanalingana na hili neno ‘Sila,’huu ndio msingi wa kuanza
maisha ambayo ni ya kidini.
Kama nyumba ikijengwa bila kuweka msingi mzuri,haitakuwa imara.Mtu wa kisasa
amegundua baada ya kutaabika sana jinsi ambavyo ni muhimu sana kuishi maisha ya
‘Sila’ Ina maana kuheshimu haki ya watu wengine kuishi.Kama tukiamini kwamba dunia
ilitengenezwa kwa ajili yetu peke yetu, basi tutachukua kila kitu kilichopo bilka kujali;
Hatutajali litakalowafika viumbe wengine, hatutajali mazingira kama vile mimea,mito,
anga, na kadhalika. Mwisho wake kwa sababu ya dosari za ekolojia zilizosababishwa na
maisha yetu ya kisasa tutajiangamiza wenyewe.Mbudha mzuri anaheshimu na anajali
wanavyoishi viumbe wengine,
Budha, kwa upeo wake mkubwa alifahamu kwamba hatuwezi kukamilika mara
moja.Kwa hiyo anaanza kwa kuituhimiza tuache kutenda matendo yenye madhara.
Tukipata maendeleo katika kuweka msingi mzuri wa maadili,tunaweza kuanza kuitakasa
akili.Ubudha unamruhusu mtu kujiendeleza kufuatana na kiwango chake cha ufahamu na
haimwekei mtu kanuni ngumu za kufuata bila kujali uwezo wake au mtazamo wake wa
maisha. Kanuni zina faida kwa kukuza tabia za kiutu na thawabu.Hizi ni tabia ambazo ni muhimu
sana kudumisha amani na furaha. Hizi kanuni zinatakiwa kufuatwa sio kwa kuogopa
adhabu lakini kwa ajili ya hekima na huruma. Budha alipotushauri, “Tusifanye
uovu,”ilikuwa ni kwa faida ya watu wengine.
Kama binadamu, ni wajibu kuwasaidia wengine kwa kutenda ukarimu,kwa wema,na
kuwapa msaada wengine wanaohitaji msaada wetu kuondoa mambo
yanayowasibu,mashaka na matatizo mengine.Kwa kutoa msaada kwa wengine bila
ubinafsi, sio tu tunawasaidia wengine,bali pia tunaupunguza ubinafsi wetu. Tusifanye
tendo jema huku tukiwa na hila moyoni,kwa sababu tendo letu zuri litaharibiwa na
ubinafsi na hizo dhamira mbaya.
Kwa hiyo maana halisi ya dhana ya Kibudha ya ‘kuacha kutenda uovu’ na ‘kutenda
mema’haitegemei adhabu au zawadi,isipokuwa lengo lake ni kuzipunguza tabia zetu za
ubinafsi ili tuongeze usafi wa mawazo.Hatutumii vitisho kuwafanya watu wazingatie
kanuni.Kutumia vitisho badala ya kuwaelewesha watu hakutawafanya watu wawe na
hisia ya huruma, na badala yake unawezakuwafanya watu wawe washirikina au wawe
watu wanaotii kauli bila kuuliza maswali.
Kuepuka uovu na kutenda mema,ni mambo mazuri sana,lakini hayatoshi.Kutokana na
uzoefu tunafahamu kwamba ikiwa bado uchu,hasira na kuduwaa kumejichimbia sana
ndani ya akili, bado tutakuwa tunaweza kutenda matendo mabaya kwa hiyo ipo haja
kwetu sisi kuitakasa akili. Kufanya hivi itabidi tuilinde akili yetu na tuyaondoe mawazo
yoyote yale ambayo ni machafu. Iwapo mawazo na dhamira chafu zitazimwa,akili daima
itakuwa safi na yenye wema, na tutakuwa tumelifikia lengo letu la mwisho.
Lakini kama binadamu,tunafahamu kwamba maisha yetu tunayoishi siyo ya kwanza na
ya mwisho. Faida ya kuwa binadamu ni kwamba tunalifahamu hili na tunaweza
kujitayarisha kwa maisha ya baada ya kifo. Watu wengi wanatumaini kwenda mbinguni
baada ya kifo lakini tunavyoona jinsi dini zingine wanavyoielezea tunalazimika kufikia
uamuzi kwamba hawajui ni kitu gani au iko wapi au ufanye nini ili uzipate starehe za
mbinguni? Hata unavyoishi hapa duniani unaweza kuzipata starehe za mbinguni. Wakati
tajiri fulani alipouliza ushauri wa Budha jinsi ya kwenda mbinguni baada ya kifo,Budha
alimjibu, “Wewe ni tajiri. na bado unauliza ufanye nini ili uzipate starehe za mbinguni?
Kwa nini unataka usubiri mpaka utakapokufa ndipo uzipate starehe za mbinguni?Hata
unapoishi hapa duniani unaweza kuzipata starehe za mbinguni kama utayatumia maisha
haya vizuri.. “
Budha alikuwa mwalimu mzuri wa dini ambaye hakutaka kuingiza ushirikina ,vishawishi
au woga katika maisha ya watu.Watu lazima wajifunze jinsi ya kuyatumia haya maisha
vizuri,wajue jinsi ya kuepuka matatizo,vurugu,migogoro,mashaka na karaha,ili wapate
elimu zaidi na hekima.Baada ya kuiendeleza hekima,wataweza kuyarekebisha maisha
yao.
FURAHA YA MWILI NA YA AKILI
Ingawa vurugu nyingine haziwezi kuwa dhahiri kwetu, mawazo fulani ya kiovu
yaliyojichimbia sana katika akili yanaweza kuwepo.Wakati fulani tunaweza kuwa
kimya,na kuwa na sura ambayo haijakunjamana kwa vile hakipo kitu chochote
kinachotsumbua; lakini kama vurugu fulani ikitokea,hali yetu inabadilika tunakuwa na
ghadhabu na sura yetu inakunjamana. Ile furaha ya mwili ambayo kwa muda inatokea
katika akili tunaidhania kwa makosa kuwa ndio furaha ya kweli.Lakini sio hasa furaha ya
kweli. Furaha ya mwili ni kutosheka tu kwa hisia. Tabia ya furaha ya mwili ni kwamba
inatoweka baada ya muda kidogo Kutafuta furaha ya mwili kusifananishwe na kutafuta
furaha ya akili. Furaha ya mwili haidumu, inapiga chenga nyingi,na baada ya kuondoka
inakuwa chachu. Pia, inaweza kuwa na gharama, ingawa hairidhishi, lakini furaha ya
kweli sio hivyo,yenyewe hainunuliwi,inatoka katika chanzo cha ndani ya akili, na
inadumu muda mrefu.
Starehe ya mwili tunayoipata wakati huu inatuhadaa kwa sababu haidumu. Wakati huo
huo, hatuwezi kuwa na furaha kwa kudumisha hitilafu za mawazo kama vile
woga,hasira,husuda, uhasama na nia ya kudhuru. Wakati hayo mambo hayapo akilini,
basi ule uangavu unaotokea kwa muda katika akili ndio tunaita furaha.
FURAHA INATOKANA NA MATENDO MEMA.
Ili kuwa na furaha tunatakiwa kutenda matendo mema zaidi na zaidi.Maana ya matendo
mema ni kutoa msaada fulani kwa wengine ili kuyaondoa mateso yao. Furaha
tunayoipata kwa kutenda mema ni muhimu kuliko kulimbikiza mali.Kila tunapofanya
tendo jema kwa imani na ufahamu,tunapata furaha na tunajisikia vizuri.Hii ndio tunaiita
thawabu. Hali ya akili tunavyoiendeleza katika maisha haya inaamua maisha tutakayoishi
baada ya kufa.Baada ya kufa hakuna kitu chochote kinachoweza kutusaidia isipokuwa
thawabu au karma.Kwa hiyo lazima tujitahidi kwa kadiri tuwezavyo kufanya wema
katika maisha haya kwa sababu ndio pekee bima yetu ya kuhakikisha kwamba tunazaliwa
upya katika maisha ya bahati.
Wapo watu fulani wasiokuwa na ufahamu ambao wanaweka vitu vya thamani katika
jeneza kwa kufikiria kwamba itamsaidia mtu aliyekufa. Lazima tuitumie akili yetu na
tuelewe mambo bila tu kufuata tabia za kizamani za waliotutangulia. Muda umefika wa
kuziacha tabia hizi ili tusilaumiwe na watu wa dini nyingine ambao watafikiria hizi ni
tabia za Kibudha.Budha kwa mfano hakuwataka wafuasi wachome kitu chochote kwa
ajili ya watu waliokufa. Alitushauri kuzichoma moto takataka za akilini.
2. SAMADHI KWA KUPITIA KUTAFAKARI
Samadhi ndio msingi wa pili, kuyakusanya mawazo au kuiendeleza akili ili kupata amani
na shwari kwa kuidumisha akili ili ifikirie mada moja tu.Akili za watu ambao hawana
uzoefu kama huu ni dhaifu sana. Akili zao ni dhaifu kwa sababu woga unawasumbua.
Tunazo hisia za kujiona kwamba hatuko salama,kwamba hatuna kinga ya kutosha,na kwa
ajili ya huo udhaifu tunajishuku.Kila dakika, nguvu zetu za akili zinapotea bila faida yoyote, kwa kupitia hisia zetu tano. Hizi hisia zetu tano zinaitoa nje nishati ya nguvu yetu
ya akili, na zinazitumia hizo nguvu kukaribisha vitu ambavyo vinatuletea wasiwasi, woga
na mashaka. Wakati huo huo vinaweza kuunda kinachoonekana kuwa ni kuridhika kwa
hisia au msisimko, Hatimaye kwa njia hii, tunaivuruga akili. Tunakusanya vitu visivyofaa
kutoka nje kupitia hizi hisia tano, na tunaichanganya akili yetu. Kwa hiyo akili inakuwa
haina muda wa kupumzika na inakuwa dhaifu kwa ajili ya huku kupotea kwa nguvu. Ni
kama maporomoko ya maji ambayo yanaendelea kutiririka na kueneza maji kila pahali
kwa sababu hakuna njia nzuri ya kuyaongoza maji yatumike vizuri. Lakini boma inaweza
kujengwa kutengeneza umeme ambao unaweza kutumika kwa kazi tofauti nzuri.
Injinia , baada ya kuona kwamba kuna hasara kubwa ya maji yanayoporomoka anaamua
kujenga boma kuyavuna hayo maji na kutengeneza umeme unaotokana na nguvu ya maji,
ili kuliangaza bonde lote. Kwa njia hii hii, tunapoteza nguvu zetu kwa vile hatayakusanyi
mawazo yetu. Budha alitushauri tusizipoteze nguvu zetu kwa kupitia hizi hisia tano,
isipokuwa tuipumzishe akili, ili isilazimike kufanya uamuzi kila wakati kutokana na
habari zinazotokana na hisia hizi tano. Ni usumbufu, mkubwa sana kwa akili Katika kile
kipindi cha kupumzika kwa akili, tunaweza kufikiria mada moja tu, bila kuiruhusu akili
kuirukia mada hii au ile.na kwa hivyo tutaweza kuiendeleza akili yetu. ‘Bhavana”
maana yake kuiendeleza akili, yaani kufanya akili ikusanye na kuivuna nguvu
inayopotea na ijiumbe upya.Akili ikikua kikamilifu,inakuwa na nguvu kubwa,na woga
wote,wasiwasi wote,na hisia zote za kujiona uko hatarini zitatoweka.Halafu utakuwa na
ujasiri,elimu na hekima. Ili tudumishe maadili,lazima tutafakari,ambayo ndiyo
inaitwa’samadhi’ Samadhi ni hali ambayo akili inakuwa shwari. Akili ambayo
haijanidhamishwa ina tabia ya kwenda huku na huku na siyo rahisi kuimiliki na inaweza
kufuata wazo au taaswira yenye madhara makubwa Ili kuizuia hii tabia mbaya ya akili,
mawazo ni lazima yakusanywe ili akili ifikirie mada moja tu,
Na baada ya muda,pole pole akili inaweza kudumu katika mada moja.,kama
inavyoelekezwa.Kwa kuchagua mada fulani,inawezekana kuuondoa udhaifu fulani wa
akili.Kutafakari siyo kuifikiria mada yoyote maalum, Kutafakari ni kuiweka wazi akili ili
iweze kufikiria mada moja.Lakini kwa kufikiria mada fulani unaweza kuuondoa udhaifu
fulani,Kwa mfano ukitafakari kuhusu urafiki,unaweza kuyaondoa makali ya
uadui,gadhabu na husuda.Ukitafakari kuhusu sehemu za mwili ambazo ni chafu au zenye
magonjwa,unaweza kuiondoa tabia ya ngono.Ukitafakari kwamba siku moja
utakufa,labda utachangamka na kufanya kazi kwa bidii,na hutaridhika na mafanikio
uliyoyapata.Ukizitafakari tabia nzuri za Budha,unaweza kuondoa kukata tamaa ya
maisha,wasiwasi na mawazo ya kutojiamini.Kwa kukuza huruma,mtu anayasahau
matatizo yake mwenyewe na anaona kwamba wapo watu wengi wenye matatizo.
Kwa kuendelea na mazoezi ya kutafakari Budha na wafuasi wake waliweza kupata
uwezo mkubwa wa akili. Waliweza kuondoa kabisa uchu,chuki na kuzumbaa.Iwapo
tunataka furaha tujifunze jinsi ya kuipumzisha akili na kuiendeleza na kuzing’oa kutoka
kwenye mizizi yake nguvu za uovu zilizomo ndani.
Wakati ule tunapotafakari,tunakuwa na amani lakini mara tu tunapoacha kutafakari na
kurudia katika hali yetu ya kawaida ya kufikiri,amani na furaha vinatoweka,na vurugu inarudi.Maji katika dimbwi yanaweza kufunikwa na majani mengi juu,lakini kule chini
maji ni masafi,ukiyasogeza majani kwa mkono,utayaona maji masafi chini,lakini
ukiuondoa mkono wako majani yatarudi.Kutafakari kunasaidia kuyaonyesha’maji masafi
ya akili’Mwangaza kamili ni wakati ambapo majani yanaondoka moja kwa moja.,na
maji yanakuwa masafi moja kwa moja.
Tunapotafakari akili yetu inatakasika.Hii ni kwa sababu hatuyaruhusu mawazo maovu
kuiviruga akili yetu..Kwa njia hiyo hiyo,tunapoacha kutafakari,mawazo maovu yanaanza
tena.
Tukiyafunika na ndoo majani ya kijani kwa muda wa wiki tatu halafu tuyafunue
tena,tutaona yamebadilika rangi. kwa ajili ya kukosa mwangaza wa jua Na
tunapotafakari,mabadiliko mengi yanatokea katika akili.Tunakuwa shwari bila hasira
yoyote kwa sababu akili yetu inakuwa katika taathira nzuri ya mkusanyiko wa
mawazo.Lakini tukiirudia tena hali yetu ya kawaida ya maisha,mawazo yale yasiyofaa
yanarudi,kama vile yale majani yanapofunikwa yanabadilika rangi kwa sababu
mwangaza wa jua haupiti.Kwa hiyo upo umuhimu wa kuiendeleza akili ili isirudie katika
hali ya kuchanganyikiwa.Lengo la kutafakari ni kukusaidia kuiwezesha akili daima
ibakie katika hali ya kutakasika.
ELIMU NA HEKIMA
Hekima sio elimu.Tunapata elimu baada ya kusikiliza,kusoma,na kuyaangalia mambo
mengi katika dunia hii,lakini sio hekima hasa.Hekima inatokea katika akili wakati
vipingamizi vya akili,vizuizi na vikwazo vingine vinapoondoshwa. .Kuna wasomi wengi
duniani ambao,bila shaka,wanayo elimu nzuri lakini kwa bahati mbaya hawana hekima
sahihi.
Watu wengi wana akili lakini vitendo vyao havina mantiki,kwa sababu wana hasira za
karibu,wana maringo,wana hisia zinazolipuka upesi,wana uchu,wana hisia
zinazobadilika mara kwa mara.Kwa upande mwingine,kuna watu wengine ni wapole,na
ingawa wana subira,uvumilivu na tabia nyingine nyingi nzuri,hekima yao siyo nzuri na
wanaweza kupotoshwa kwa urahisi na wengine.Tukiwa na ukarimu bila
hekima,tutajiletea matatizo kwa sababu watu wengine watakuwa wanatuomba hela kila
wakati.Kwa hiyo hekima na thawabu lazima viwe pamoja.
KUWA HURU KWA KUTUMIA HEKIMA
Panna..Hekima ni hatua ya tatu na ya mwisho katika njia.Baada ya kuzingatia
maadili,mfuasi anajifunza kutafakari.Mawazo yake yanapokusanyika,anakuwa na uwezo
wa kuelewa jinsi vitu vilivyo hasa.Hekima ni kuielewa dunia vyema kwamba
haidumu,hairidhishi na siyo ya kukumbatiwa.Elimu ni aina tatu,a)ile inayopatikana
kutokana na kujifunza,b)ile inayopatikana kwa kufikiri,c)ile inayopatikana kwa
kutafakari.Hii ya mwisho ndiyo kilele.Inamwezesha mtu kuifikia nirvana.
Kuzumbaa,ujinga,na mawazo maovu yanapotoka akilini,uangavu unatokea badili
yake.Huu uangavu ndiyo hekima.Kila tunapozidi kujifunza mambo ya kidunia na akili
iliyozubaa,ujinga wetu unaongezeka.Akili ikifunguka kikamilifu maendeleo yanaweza kutokea,na hapo tu ndipo hekima na na ufahamu na utakaso vinatokea katika akili.Haya
ndiyo maendeleo ya ndani.
Hatuwezi kuuleta huu uangavu,utakaso na ufahamu kutoka nje.Ni lazima utoke ndani
.Sila,Samadhi.,Panna-mazoezi haya ya akili ndiyo misingi mitatu mikuu ya Kibudha ya
kuizoeza akili. Maendelezo zaidi ya akili kwa madhumuni ya kupata ukamilisho yanaitwa
Adhi Sila. Shwari ya akili inaitwa Adhi Citta(Samadhi).Kupata hekima ya juu kwa
kuendeleza ufahamu kunaitwa Vipassana.,ambayo pia inaitwa Adhi Panna.Kwa hiyo,hii
ndiyo misingi mitatu mikubwa ya Ubudha ya kuizoeza akili,
MPANGO WA MAFUNZO WA MISINGI MITATU
Huu ndio mpango wa kufundisha maadili Kibudha,kwa kutumia misingi mitatu
inayotegemeana.Nazo ni sila,ambazo ni kanuni za maadili ambazo zinafuatwa kwa
makusudi na kwa hiari kubadili tabia za maneno na matendo,samadhi,kufundisha
mkusanyiko wa mawazo,na panna,kuendeleza hekima ili maadili yaweze kukamilika.Sila
ndiyo inaaminika ambapo yale mengine mawili yanajengwa. Mpango wa njia
unaonyesha kuwa Ubudha ni kitu abacho kinatekelezeka.Kukamilika kwa sila
kunatambulika kuwa ndio msingi wa kazi yote ya kiroho.Mtu mwenye akili anatakiwa
ajizatiti katika sila,.aiendeleze akili yake(citta),na aendeleze hekima(panna).Mtu kama
huyo anaweza kujinasua kutoka kwenye nyavu za uovu.
http://deniceshonko.blogspot.com/2012/04/makala.html
http://deniceshonko.blogspot.com/
Kazi Bomba sana. Ama kweli, Hekima sio elimu.Tunapata elimu baada ya kusikiliza,kusoma,na kuyaangalia mambo
ReplyDeletemengi katika dunia hii,lakini sio hekima hasa.Hekima inatokea katika akili wakati
vipingamizi vya akili,vizuizi na vikwazo vingine vinapoondoshwa. .Kuna wasomi wengi
duniani ambao,bila shaka,wanayo elimu nzuri lakini kwa bahati mbaya hawana hekima
sahihi.
Hakuna nishati ambayo inaweza kulingana na akili ya binadamu, Akili ndio
ReplyDeletemtangulizi wa kila kitu, akili ndio inayoongoza na vitu vyote vinavyo chanzo
chake katika akili.. Budha amesema , ‘ Siifahamu nishati nyingine kubwa kuliko
akili ya binadamu ambayo inaweza kukimbia mbio sana,. Kwa mfano wale ambao
wamesoma sayansi wanaweza kuelewa mara moja umbile la atom. Atom
inabadilika mara milioni chache katika muda wa nukta moja.