Menyu

Swahili Hub

Mbinu za Lugha ya Kiswahili


Mbinu za Lugha
Katika fasihi, mwandishi au msimulizi anaweza kupitisha ujumbe wake kwa njia mbali mbali zinazomwezesha kuwasilisha ujumbe wake vizuri na kwa lugha inayopendeza. Kuna tanzu mbili za mbinu anazotumia mwandishi/msimulizi wa fasihi:
a) Mbinu/Fani za Lugha 
b) Mbinu za sanaa
Mbinu za lugha hutambulikana moja kwa moja kutokana na uteuzi wa maneno yaliyotumika. Msomaji hahitaji kusoma kifungu kizima ndipo mbinu hiyo ijitokeze.
Mbinu za sanaa humhitaji msomaji asome kifungu kizima, au hadithi yote ndipo mbinu iliyotumika ijitokeze.
{Mbinu za Lugha ya Kiswahili}


A: MBINU ZA LUGHA

1.    Tanakali za Sauti 
Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
 Mfano:

Anguka pa  
Anguka mchangani tifu          
Tumbukia majini chubwi                    
Lia kwi kwi kwi
Tiririkwa na machozi tiriri tiriri              
tulia tuli                                
Bingiria bingiribingiri                          
nyooka nywaa
Kuwa mweupe pe                                 
mweusi tititi


Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha;  'kama', 'mithili ya', 'sawa na'

 Mfano:
mweusi kama makaa                      
 mweupe kama theluji              
mrembo mithili ya malaika                
baridi kama barafu        
pumbafu kama kondoo                    
mwembamba kama sindano  
maridadi kama kipepeo                  
mtundu kama tumbili
pendana kama chanda na pete                                                            
adimika kama maziwa ya kuku

3.    Tashihisi/uhuishaji (personification)
Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu)  
Kwa mfano:      
·         picha hii imekuwa ikinikodolea macho tangu asubuhi
·         Fikira zangu zilikuwa zikizunguka kwenye ajali niliyoshuhudia siku hiyo,
·         Upepo mkali umeyafukuza mawingu yakatoweka angani na sasa jua linatuwanga kwa hasira.
 4.    Takriri (repetition)
Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani.
Kwa Mfano:          
Tumechoshwa na siasa mbaya. Tumechoshwa na ahadi zisizotimizwa. Tumechoshwa na miradi isiyo kamilika. Tumechoshwa na malumbano na migogoro ya kikabila. Tumechoka.
Hongera hongera Bwana Kisaka, hongera kwa ujasiri wako. Hongera! uliyoyatenda ni raha kwetu. hongera

5.    Istiara (imagery)-      
Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo 'ni' ama 'kuwa'

·         Mama wa kambo amekuwa mamba, nyumbani hamkaliki          
·         Dassa ni mkono birika, hatakupa utakacho
·         Masomo nayo yamekuwa mawe

6.    Taswira – 
Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.

Chumba kilikuwa kimepambwa kikapambika. Macho yangu yalitua kwenye pazia iliyoning'inia karibu na kitanda. Mkabala wa kitanda palikuwa na meza iliyowekelewa redio iliyocheza kwa sauti ya juu. Saa kubwa ya ukutani ilining'inia juu ya meza....

7.    Jazanda - 

Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.

Mfano:
Mama wa kambo anatuhangaisha sana. Ni heri kuishi bila makazi kuliko kukaa nyumba moja na simba huyo.

8.    Majazi
 ni mbinu ya mhusika kuwa na jina lake rasmi (jina la kuzaliwa) linaloambatana na tabia/mienendo/sifa zake.
 Kwa mfano:
Mhusika Bahati katika riwaya; ikiwa maisha yake yatadhihirisha kuwa na bahati nyingi; basi hiyo itakuwa ni mbinu ya Majazi.

9.    Lakabu – 
ni mbinu ya mhusika kupewa/kubadikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
 Kwa mfano:
Mhusika Ali katika riwaya ni mwalimu mkali sana anayeogofya wanafunzi wake; kutokana na ukali wake wanafunzi wanambandika jina ‘Mamba’ na jina hilo linakomaa. Jina la Mamba litakuwa jina la lakabu.

Katika kitabu cha Siku Njema, mhusika mkuu anabandikwa jina Kongowea Mswahili kutokana na ujuzi wake wa Kiswahili.

10. Chuku (hyperbole)– 
Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani.
 Mifano

·         Alilia akadondokwa na machozi mengi yaliyomlowa mwili mzima, na kutiririka hadi yakaunda kijito cha maji
·         Kabla ya kifo cha mama Kajuta, alikuwa amekonda akabaki mifupa pekee.
·      
11. Nahau/Misemo – 

Nahau na misemo hutumika kupitisha ujumbe wa mwandishi kwa kutumia maneno ambayo hayamaanishi katika hali halisia. Misemo hutumika sana katika fasihi na katika mazungumzo ya kawaida ili kufanya lugha iwe ya kupendeza. Aidha, nahau na misemo hutumika kupunguiza makali/machukizo ya maneno katika kupitisha ujumbe uo huo.

Tofauti kati ya misemo na nahau ni kwamba nahau huchukua kitenzi ilhali misemo ni virai visivyo vitenzi

Mifano ya nahau
Kupiga moyo konde      -           kujituliza/kujiliwaza                        Kujipa moyo                 -           kujiliwaza
Kupiga hatua               -           kuendelea mbele                            Kukata kamba             -           kuaga dunia
Kupiga darubini            -           kufanya uchunguzi                        Kutupa macho              -           kuangalia mbali
Kupigwa kalamu          -           kufutwa kazi                                  Kuandaa meza             -           kutayarisha chakula
Kugonga mwamba       -           kutofanikiwa                                   Kwenda msalani         -            kwenda chooni

Mifano ya Misemo

Mkono wa birika           -           uchoyo                                        uzi na shindano     -    ushirikiano
Shingo upande             -           bila kupenda                                kiguu na njia        -     kupenda kurandaranda
Mdomo na pua           -           karibu sana                                   Lila na fila                    -           mema na mabaya

12.  Maswali ya Balagha/Mubalagha (retorhical questions)
Mhusika au msimulizi huuliza maswali yasiyohitaji majibu.
Mbona nateseka daima? Nilimfanya nini kilichomfanya Maulana kunitupa milele?

13. Uzungumzi Nafsiya - 

Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
Mfano:

Musa: (baada ya kuteteshwa na mwajiri wake) Inavyoelekea ni kwamba nitaipoteza hii kazi, lakini sitakufa moyo, ninajua hatua nitakayochukua.

14. Ritifaa
Kuzungumza na mtu aliyekufa.
Kwa mfano
Baba ooh Baba, mbona umeniacha nikihangaika? Ulipokuwa hai nilikula na kushiba, nilivaa vizuri lakini sasa tangu uende ninateswa na kukandamizwa. tafadhali baba rudi. Toka kaburini uniokoe.

15. Utohozi wa maneno
Ni kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.
Mfano:

Hata kama hautanikuta katika ofisi, hakikisha umempa sekritari stakabadhi zote.
Skuli zikifungwa ningetaka wewe na bratha yako mje kunisalimia.

16. Kuchanganya Ndimi

Kuingiza maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.

Kwa mfano
Nimempigia waziri simu na amekubali kunipatia hiyo contract kuanzia next month.
Kasuku hapatikani nyumbani kila kunapo wedding ceremony katika kijiji hiki.

17. Kuhamisha Ndimi

Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.

Kwa mfano
18. Methali
Mbinu ya wahusika au msimulizi kutumia methali kama mapamabo ya lugha katika masimulizi

19. Kejeli
Ni kutumia lugha inayoonyesha kudharau au kufanya kitu kiwe kidogo sana kuliko kilivyo.

20. Ukinzani
ni kutumia maneno yanayopingana kimaana au yaliyo kinyume ili kusisitiza ujumbe.
Mfano: wazee kwa vijana, wake kwa waume;
liwake lisiwake kutakucha twende zetu
Nitakuchukulia hatua ya kisheria upende usipende


MBINU ZA SANAA

mbinu za kisanaa hutambulika baada ya msomaji kusoma kifungu kirefu katika riwaya.

Kinaya  (irony) - Kinaya ni hali ya mambo katika riwaya/hadithi kuwa kinyume na matarajio.

Kwa mfano: Kiongozi fulani kujisifia kwamba yeye ni mpenzi wa watoto na wanawake ilhali ni yeye anayeendeleza unyanyasaji wa wanawake na watoto.

Taharuki (suspense) - ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kutumia maneno na kujenga hali inayozua hamu kwa hadhira; hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza.

Sadfa (Coincidence) - Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa japo havikuwa vimepangiwa. 

Kwa mfano: mhusika fulani akiwa katika mawazo ya namna atakavyopata pesa; rafiki yake anamtumia pesa jambo ambalo halikutarajiwa.

Mbinu Rejeshi/Kisengere Nyuma (Flashback) - mwaandishi husimulia hubadilisha wakati wa masimulizi na kusimulia namna kisa kilivyokuwa wakti fulani uliopita.
Mfano:
Mhusika Y wanakutana na Mhusika Z. Kisha kila mmoja anamtambua mwenzake. Wanaanza kukumbuka maisha yao ya utotoni, namna walivyojuana. Ikiwa mwaandishi atabadilisha wakati wa masimulizi kutoka wakati ambao wahusika hawa wamekutana hadi wakati wa utotoni wao, basi hiyo itakuwa ni mbinu rejeshi.

Kisengere Mbele/Utabiri (Flash Forward) -
Mwandishi anapobadilisha wakti na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni,kabla ya kuwa, huwa anatumia mbinu ya utabiri.
Mfano:
Sara na Saidi walilelewa pamoja, wakicheza pamoja, wakasoma pamoja wala hawakujua kwamba watafunga ndoa siku za usoni.
Njozi au Ndoto

Upeo wa Juu (Climax) na Upeo wa Chini (anticlimax)

Wimbo

<<<<
Powered by Disqus

0 comments:

Post a Comment