UNAHISI
mwenzi wako anakusaliti kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume
wengine? Fahamu kuwa wapo wengi wenye kulalamikia hilo.
Kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa
aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na
kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye
kumpendeza mwingine.
“Mimi
najitahidi kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo
baadhi ya watu wanavyojisemea.
UKWELI
UKOJE?: Ni vizuri katika mapenzi kupata muda wa kuzungumza mwenzangu
unapendelea nini na usingependa ufanyiwe nini.
KUAMINI
KUWA UNAYOFANYA NI MAZURI, BILA KUAMBIWA NA UNAYEMFANYIA, SIO SAHIHI.
Maisha
ya raha katika uhusiano ni kuhakikisha kunakuwa na fursa ya wapendanao kukaa na
kujadili namna gani wamekuwa wakiishi na nini cha kufanya ili waweze kuwa na
maisha bora zaidi.
KUKWAZANA
NI MAMBO YA KAWAIDA KATIKA MAPENZI. IKIWA UMEKAA KWENYE TUMBO LA MAMA YAKO NA
BADO KUNA WAKATI MNAKWAZANA, IWE MTU AMBAYE MMEKUTANA TU MITAANI?
Jambo muhimu katika ndoa ni kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya wanandoa
kujadili hali ya ndoa yao.
Kama
ilivyo katika biashara kwamba wafanyabiashara wakati fulani wanajadili hali ya
maendeleo ya biashara ili kujua kama kuna matatizo gani nk, ni muhimu sana
wanandoa kutenga muda wa kujadili hali ya uhusiano wao.
SABABU
ZA WATU KUSALITI
Wakati fulani nimekuwa
nikiongea na watu wanaosaliti ndoa...baadhi yao ukiwauliza unaonaje sasa
ukaondoa kwenye ndoa na kuoana na huyo wa nje, jibu ni kwamba hawezi kwa sababu anasaliti si
kwa sababu hampendi aliyenaye, bali wakati mwingine ni kutofautiana.
Kwa
mfano katika utafiti wangu nimegundua kwamba idadi kubwa ya wanandoa waume,
hawana uhakika wa kupata tendo la ndoa kwa wakati wanaotaka, kama ilivyo kwa
baadhi ya wanawake.
Tafiti
ambazo nimekuwa nikifanya pia nimegundua kuna tofauti ya mahitaji katika ndoa,
kwa mfano wakati wanaume ni wenye kuhitaji mno tendo la ndoa, furaha ya
wanawake walio wengi sio hilo wakati fulani ni uhakika wa kupatikana kwa
mahitaji ya ndani na amani.
*Kutopata
mapenzi ya kweli katika ndoa hasa ikiwa Kijana/Binti alilazimishwa kuoa/kuolewa
na mtu ambaye hakumpenda.
-Wengine
hawapata mapenzi ya kweli kwa sababu tu mwanaume au mwanamke hamjali, kitendo
ambacho kinasababisha baadhi
yao kuona kwamba suluhu pekee ni kwenda nje ya ndoa.
*Uchafu,
kutojijali au kujipenda kwa mwanaume na mwanamke
-Wapo
wanaume na wanawake ambao wamekuwa wachafu wa mwili na kutojipenda, kiasi
kwamba ukiwa nae unahisi kichefuchefu. Kuna wanaume na wanawake kwa mfano wanalala bila
kuoga, wengine unakuta mwingine mlevi, mwingine hanywi, kisha anarudi nyumbani
anaomba abusiwe...mhh! raha iko wapi hapa?
*Kutotosheka/kuridhika katika tendo la ndoa
-Ingawa
wakati mwingine huwa ni uroho wa mtu, mara nyingi hata majumbani watoto kama
hawajashiba, baadhi yao hukimbilia kudowea chakula kwa jirani.
*Ubize
wa kazi kupita kiasi/Kusafiri
-Kuna watu
wako bize kila kukicha, wakati mwingine si kweli kwamba wako bize bali ni unafiki au labda kutojua
namna ya kupangilia mambo. Wengine ni watu wa safari kila mara, hiyo ni mbaya
kwa wanandoa.
*Tamaa
ya mali: Kuna wengine wako tayari kufanya ngono hovyo ili wapate mali. Huu ni
ujinga, badala ya mtu kufanya kazi, anafikiri kwamba njia rahisi ni kubabaikia
wanaume wenye magari, wenye fedha nk.
*Kujifunza
mambo au mitindo mipya
-Wakati mwingine kuna wengine
wanatoka nje ili kusaka miondoka mipya...kuna wengine wamekuwa waoga wa kusema
ukweli kwa wenzi wao juu ya yale
ambayo wanayataka, matokeo yake wanaona wafanye hiyo ‘dawa mbadala’.
*Kutopata
tendo la ndoa muda mrefu, labda kwa sababu mume ana matatizo au mke ana uja
uzito mkubwa ama amejifungua n.k
-Hata hivyo
kitaalam kuna njia za kuridhishana si lazima tendo la ndoa la aina moja, bali wapenzi wanaweza
kuchezeana na kila kitu kikawa chenye kuwafurahisha wote au kumfanya mwenzi
wake afurahie.
Makala
hii itaendelea toleo lijalo, lakini ambacho unapaswa kubaki nacho leo ni kwamba
ni vizuri wanandoa kuwa watundu kwa kubuni mbinu na miondoko tofauti ya
kuridhishana.
0 comments:
Post a Comment