Mimi ni mzazi mwenye watoto wanaosoma shule za sekondari za binafsi, ingawa walichaguliwa na Serikali lakini nikaona niwapeleke huko labda watapata elimu bora, lakini imekuwa kama wanatufanya sisi mitaji.
Kila kunapokucha watoto huja na barua kutoka shule ya mchango mara wa jingo mara maabara, mara masomo ya mwezi na mambo mengine kadha wa kadha hadi unajikuta unakosa cha kuwapa kupeleka.
Lakini ukikagua madftari ya watoto hawafundishwi karibu kila siku na hata mitihani wanachelewa kurudishiwa, sasa unajiuliza fedha wanazoomba kila siku hufanyiwa nini?
Jamani kwanza ningeomba shule hizi zipunguze karo, kwani ni kubwa lakini pia kama wanatoza wanafunzi fedha za michango kila mara basi tuone juhudi zao kwa matokeo bora ya wanafunzi.
Kero hii ni ya muda mrefu ningeomba shule za binafsi zifundishe kadri wanavyotoza ada.
<<<<<
0 comments:
Post a Comment