Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

Malenga wa Mvita Ahmad Nassir


AHMAD NASSIR ni mzee mswahili wa Mombasa. Kwa upande wa babake ni Mtangana na kwa mamake ni Mkilindini. Hizi ni miongoni mwa kabila za asili ya Kiswahili za ki-mvita, yaani MombasaBwana Ahmad alizaliwa kuze, Mombasa mnamo 1936. Kama watoto wengine wa kimombasa wa wakati huo aliingia chuoni kusoma kuraani na dini ya kiislamu. Mafunzo hayo aliyapata kwa babu yake Sheikh Muhammad Ahmad Matano, mpaka alipohitimu.