Menyu

Swahili Hub

Lugha ni Njia


UTANGULIZI
Lugha imewahi kufafanuliwa kwa jumla kama mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Wataalamu wengi wa isimu (sayansi ya kuchanganua lugha na kuieleza jamii) kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86 na lugha wanaelekea kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao ( massam ba D.P.B na wenzake 1999, TUKI).


Lakini inaeleweka ya kwamba viumbe vingine navyo vinaweza kutoa sauti za aina mbalimbali na aghalabu kwa madhumuni hayo hayo ya mawasiliano viumbe hivyo vinaweza kuwa kuku, amwonapo mwewe kuna lugha au sauti anayoitumia kuashilia hatari Fulani ama mbuzi anapokuwa na mtoto .swahilihup
Cha kujiuliza hapa ni je, hizi nazo zinaweza kuitwa lugha? Aidha binadamu na viumbe vingine huweza kutoa ishara mbalimbali kwa madhumuni ya mawasiliano. Hizi nazo zimekuwa zikiitwa lugha kutokana na dhima yake ya kuwezesha mawasiliano baina ya viumbe hivyo swali linalohitaji kuulizwa tena katika hatua hii ni je ni kweli hizi zote ni lugha kwa maana ile ile?
Ili kujibu swali hili pengine ni muhimu kwanza kubainisha missingi ya tofauti kati ya lugha hizi zilizotajwa msingi mkubwa wa tofauti baina ya hizi “lugh” ni jinsi utoaji na utumiaji wa sauti na ishara husika vinavyochochewa kwa mfano inajulikana kwamba wakati binadamu kwa kiasi kikubwa hujifunza kutoa na kutumia sauti na ishara viumbe vingine vyote hutegemea mno silica zao katika kutoa na kutumia sauti na ishara. Hii ndio pengine ndio sababu humchukua mtoto wa binadamu takribani miaka mitatu kuweza kumudu lugha.

Wataalamu wamefikia kutenga aina kuu mbili za lugha. Hizi ni lugha asili na lugha unde.
Lugha asili ni ile inayohusisha mfumo wa sauti zinazotolewa kwa kutumia ala katika chemba yam domo wa binadamu.

Lugha unde kwa upande mwingine ni ile inayohusisha mfumo wa ishara anazobuni binadamu na ambazo huzitoa kwa viungo vyake vya nje kama vile mikono vidole kope za macho maandishi na vile vile nyenzo mbali mbali alizoziunda.

Lugha asili ina sifa ambazo unde haina hizi ni pamoja na:kiwango cha msingi kinachohusisha vipashio kamili vyenye maana kama vile maneno na,kiwango kingine kinachohusisha vipashio ambavyo vyenyewe havina maana lakini hutumika katika kuunda vipashio vya msingi vipashio hivi ni sauti katika lugha.
Sifa ya uzalishi kwa upande mwinginwe inahusu hasa uwezo wa binadamu wa kuunda na kuelewa idadi isiyo kikomo ya maumbo ya maneno na sentesi katika lugha yake. Hii ni pamoja na hata zile sentensi ambazo hazijawahi kutuingwa hapo kabla mifano ya uzalishi ni kama vile kutumia idadi Fulani tu za sauti kuunda maneno kadhaa kwa mfano kwa kutumia sauti t, a na o katika mipangilio mbalimbali Kiswahili upata maneno kama ota, toa tao sauti kama hizi huweza pia kuandamana na sauti nyingine katika mipangilio mbalimbali kutoa maneno mengine kama vile tako, toka, tokeza,pato,topa n.k na hadi leo hii hatujui lugha ya mnyama yeyote au lugha unde yenye sifa hizi.

Aidha sifa hizi zinazidi kutubainishia vipengele muhimu vya kitu “lugha” na kutudokeza kwamba pengine si kila njia ya mawasiliano ni lugha kwa maana ile ile.
Kwa kumalizia katika sehemu hii tumejifunza kwamba lugha inaweza kuainishwa katika makundi makuu mawili.

Lugha asili ambayo ni mfumo unaohusisha mpangilio wa sauti zinazotolewa kwa ala zilizomo kwenye chemba yam domo wa binadamu.

Lugha unde ambayo ni mfumo unaohusisha ishara zilizobuniwa na binadamu ambazo aghalabu hutolewa kwa viungo vya nje vya mwili na kwa nyenzo zilizoundwa na binadamu
Sifa kuu za
(a) (i) ni viwango viwili katika muundo wake na.
(ii) uwezo wa kuzalisha idadi isiyokikomo ya maumbo na miundo.
Sifa kuu za (b) kwa upande mwingine ni.
kuwa za idadi na aina mbalimbali kutegemea matumizi, na,
kutojulikana au kutomhusu kila mtu katika jamii.

CHIMBUKO LA LUGHA
Inawezekana kwamba kila jamii ina hadithi kuhusu jinsi lugha yake ilivyozuka. Lakini kuna hadithi kadha wa kadha kuhusu chimbuko la lugha asili zote za binadamu. Hadithi mojawapo maarufu ni ile ya biblia kuhusu vurumahi zilizotokea wakati wa ujenzi wa mnara wa babeli na kupelekea kuzuka kwa lugha nyingi. Hata hivyohadithi kama hii hata kama ina chembe ya kupelekea kuzuka kwa lugha nyingi. Haiwezi kutetewa kwa hoja za kitaalamu. Pengine hizo ziliwafanya watu walioishi babeli kutengana na kuhamia sehemu mbali mbali. Hiyo ingezusha lahaja na baadaye lugha tofauti. Kama si kwa hoja kama hii hadithi hii si chochote kitaalamu. Mnomno tutaishia tu kusema kwamba tunaamini hivyo jambo ambalo halisaidii kitaalamu.
Katika taaluma ya isimu msemo

“chimbuko la lugha “ huwa unatazamwa kwenye msingi wa fahiwa mbili kuu. Kwanza ni ile fahiwa inayozingatia hali za mabadiliko ya binadamu toka kale na kale hadi kupata lugha asili ambazo zote ni kamili na vilevile changamani kwa kiwango kinacholingana. Katika fahiwa hii pia huzingatiwa tofauti kati ya lugha asili na mifumo mingine ya mawasiliano kama ilivyoelezwa juu. Kinachoingiza mtafaruku katika fahiwa hii ni ule ukweli kwamba lugha uweza kuzuka, kukua na kufa. Fahiwa ya pili inayoongoza mtazamo wa kiisimu kuhusu chimbuko la lugha ni ile inayozingatia jinsi watoto wanavyoipata lugha. Hapa ni dhahiri kwamba hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na lugha au na uwezo wa kusema lugha Fulani tu na si nyingine. Badala yake kila mtoto anayezaliwa akiwa na lugha au na uwezo wa kusema lugha Fulani tu na si nyingine. Badala yake kikla mtoto wa kawaida anazaliwa bila lugha lakini akiwa na uwezo wa kupagta lugha yeyote ya jamii inayomlea au inayomzunguka. Aidha ili kupata lugha ni muhimu kwa mtoto kuwa miongoni mwa jamii ya watu. Haijajulikana mtoto huathilika vipi kuhusiana na lugha pale anapotokea kuwa peke yake tu mahali popote pale.

VIPENGELE MUHIMU VYA LUGHA ASILI YA BINADAMU.
Katika ufafanuzi uliotolew kwenye utangulizi mwanzoni lugha ilihusishwa na vipengele kadha kama vile “mfumo wa sauti” “sauti za nasibu” “sauti za kusemwa” “sauti za watu wa jamii yenye utamaduni mmoja n.k
Mfumo wa sauti
Katika lugha asili zote za binadamu mifumo ya sauti ujumuisha aina mbili kuu za sauti ambazo ubainishwa kutokana na jinsi sauti hizo zinavyotamkwa. Aina kuu ya kwanza ni sauti zinazojulikana kama “irabu”au “vokali” aina kuu ya pili ni sauti zinazojulikana kama “konsonanti”
“irabu” au “vokali” ni sauti zinazotamkwa bila kuwepo kizuizi kwenye mkondo wa hewa mdomoni. Kwa kawaida tofauti katika utamkaji wa sauti hizi huletwa kutokana na mdomo kubiringwa au kulegezwa na vile vile mahali zinapotamkwa sauti hizo ambako huwa ni juu au chini nyuma mbele au katikati ya chemba. Irabu ni sauti zinazowakilishwa na herufi kama vile a,e,i,o,u

konsonanti kwa upande mwingine ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu na kwa namna mbalimbali kwenye chemba yam domo. Ala kuu katika uzuiaji huu ni ulimi ambao huweza kugusishwa aju kufanywa ukaribie sana sehemu za mdomo kama vile kaakaa, ufizi, meno n.k
konsonanti nyingine hutamkwa kwa kubana mdomo na/au pua. Aidha kuna konsonsnti zinazotokea na mguno. Konsonanti zinazotokea na mguno ni zile zinazowakilishwa na herufi kama b, d, g, n.k na zisizotokea na mguno ni zile zinazowakilishwa na herufi kama f, t, s , n.k

sauti za nasibu.Idadi na aina za sauti ambazo hatimaye hutumika katika lugha ya jamii hazipatikani kutokana na jamii yenyewe kunuia au kukusudia hivyo. Ama kwa hakika huwa hakuna vikao wala mikakati maalumu ya jamii yenyewe kunuia au kukusudia hivyo. Ama kwa uhakika huwa hakuna vikao wala mikakati maalumu ya jamii kukubaliana kuhusu sauti hizo. Jammi hujikuta tu ikitumia sauti hizo ambazo, kwa kawaida huweza kutofautiana kidogo tu au sana na zile za jamii nyingine hali hii ya sauti za lugha kupatikana bila wenyewe kunuia au kukusudia ndiyo huitwa nasibu.

Unasibu huonekana pia katika uundaji wa maneno na tungo mbalimbali katika lugha. Kwa mfano huwa inatokea tu kuwa mpangilio wa sauti Fulani kwa namna Fulani kama vile katika umbo maji huunda neon hilo ambalo jamii ya waswahili hulitumia hulitumia kuita aina Fulani ya kioevu. Kitu hicho hicho huitwa kwa maneno yenye maumbo tofauti kabisa katika lugha nyingine. Maumbo haya ni kama vile water (katika kiingereza) eau (katika kifaransa), pi ( katika kiluo), ma “(katika kiarabu), amanchi (katika kihacha), n.k imetokea tu kwa jamii hizi zinatumia maneno haya kuita kitu hicho na hakuna anayeweza kudai kwamba neon lake ndilo hulandana na kitu hicho kuliko maneno ya jamii nyingine.
Sauti za kusemwa

Maelezo kuhusu vipengele vilivyotangulia yanasisitiza umuhimu wa sauti katika lugha asili ya binadamu jinsi zinavyotolewa na vile vile kupangika kwake hadi kuunda maneno na sentensi. Aidha imedhihirika kwamba huwa kuna utoaji wa sauti na utoaji tu wa sauti na utoaji wa sauti kwa mpango maalum. Aina ya kwanza ya utoaji wa sauti mara nyingi hauna maana yeyote na hivyo kwa kawaida hauhusishwi na kitu “lugha” aina ya pili ya utoaji wa sauti ambayo ujulikana pia kama “kusema” ndiyo sifa maalumu ya lugha asili, na kwa hakika ndiyo sifa kuu inayobainisha lugha asili ya binadamu na “lugha” nyinginezo. Aidha kitendo cha kusema ndicho huwa cha mwanzo katika mfululizo wa taratibu za upatikanaji wa lugha na matumizi yake. Taratibu nyingine kama vile uandishi na matumizi ya ishara nyingine hufuata baadaye na si kwa watu wote katika jamii. Ni dhahiri pia kwamba hizi njia nyingine haziwajkilishi lugha kikamilifu. Kwa mfano, hadi leo hii hakuna mfumo wa uandishi unaowakilisha lugha kikamilifu kabisa. zaidi ya kushindwa kwa njia hii kuwakilisha sauti zote kwa namna inayorizisha, huwa pia haitoi nafasi kwa vipengele vingine vya lugha kama kiimbo, shadda n.k . hii ndiyo imefanya wataalamu mbalimbali duniani kuita lugha ya kusema kuwa ndiyo lugha ya msingi. Taratibu nyingine kama vile uandishi huwa ni za kujaribu tu kuwakilisha lugha hii ya msingi.
Sauti za watu wa jamii yenye utamaduni mmoja.

Lugha inafungamana sana na na jamii ya watu. Na kwa kuwa lugha huwa ni kwa ajili ya mawasiliano yote katika jamii, ni dhaili kuwa inabeba na kuakisi mambo mengi ya jamii husika. Mambo mbalimbali ya jamii ndiyo huwa kiini cha utamaduni wa jamii hiyo. Utamaduni hujumuisha mambo kama fikra na falsafa ya jamii na vile vile namna mbali mbali jamii inavyoendesha mambo yake. Aidha kuna ukweli kwamba lugha ndiyo msingi mkuu wa ubunifu (wa fikra na mambo mengine) na wa utoaji wa maelekezo vitu ambavyo ni muhimu kwa jamii yoyote ile. Zaidi ya hayo lugha katika maumbile yake fulani Fulani huweza kudhihirisha vipengele vinavyoakisi msimamo au mtazamo wa jamii juu ya mambo mbalimbali. Kwa mfano uainisho wa majina ya vitu katika lugha mbalimbali hudhihirisha mitazamo tofauti ya jamii yenye lugha hizo kuhusu vitu hivyo. Wakati mathalani lugha kama kifaransa, kiarabu na nyinginezo huainisha majina ya vitu kwa msingi wa kijinsia (yaani kama cha kike ama cha kiume) lugha nyingine kama zile za kibantu huainisha vitu kwa msingi wa dhana mbalimbali tofauti. [Mengi ni hapo baadaye]

0 comments:

Post a Comment