Menyu

Swahili Hub

PENDO LA SIRI. [23/05/2012]


PENDO LA SIRI.
[23/05/2012]

Hayo ya hayawi hayawi, yaliniangukia kama nanga. Kiza kilichojimwaya kati ya upenyu wa mwanga katika aushi yangu. Yapo niliyoyaamini; Anenae kuwa pendo, si faida ni uvundo. Huyo yu katika mwendo, wa ujinga na ubaya. Na'mi kwa ari ambayo sikufahamu mwanzo wake, nikatii amri yakuwa tupendaneni, tusitendeyane ubaya...

Ama kwa hakika yalianza kama mchezo. Mara 'My son', mara wavutia mara sijui nini:- almuradi niliungulika na mengine kuyatia asali bandia. Nikajitia upofu kwa dhana kuwa mapenzi ya mtandaoni
hayana mizizi wala mashiko. Nilijizuga! Kumbe ulikuwa mwanzo wa kujitia silisili za pendo na kisha kuambua nyayo mwenyewe hadi kwenye korti la maamuzi... Nilibanwa. Nilijaribu kushikamana niwezavyo ela hamna lililonipa dalili ya kuwa waa. Nilisita nikasonga. Nikatamani kujicheka nikalia; ndani kwa ndani. Nilitamani kumcheka yeye lakini nikaishia kujipa kwikwi na shake zangu...

Kiwiliwili chake kilinitia mbioni si la siri! Mtego wake labda ulikuwa umeshasepetuka na kuninasa....Nakupa iliyo wazi, umuamini na M'ngu. Waniatia majonzi, sikitiko na tewengu. Wasafiri laazizi, wenda nayo roho yangu....[itaendelea kesho]


2 comments:

  1. Fumbo hili bona sielewi.Ndugu yangu, katokea lini haya ?

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete