Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

Jifunze Fasihi


Fasihi kama dhana, imeelezwa na wengi kwa kuegemea nadharia na mitizamo
mbali mbali.  Hata hivyo ni muhimu tufahamu ya kwamba maana inayopewa dhana au
kitu fulani, huwa inachukuana na matumizi ya dhana yenyewe, watu wanaohusika,
mahali dhana hiyo inamotokea, na hata kipindi au wakati husika.  Hii ndiyo sababu
twapata maana mbalimbali zikitolewa kuhusu fasihi.  Kwa mfano, waandishi wengi wa
Kimagharibi wamesisitiza kwamba fasihi yahusu tu kazi zilizoandikwa.