Menyu

Swahili Hub

Waandishi Mashuhuri wa Vitabu

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe. Hadithi zilizochaguliwa ni Tropical Fish (Samaki wa Nchi za Joto) iliyoandikwa na Doreen Baingana kutoka Uganda, The Madman (Kichaa) iliyoandikwa na Chinua Achebe kutoka Naijeria, na In the Cutting of a Drink (Katika Kutiliwa Kinwaji) iliyoandikwa na Ama Ata Aidoo kutoka Ghana. Hadithi ya Muhammed Said Abdulla” Mke Wangu” ambayo ni hadithi ya zamani sana iliazimwa kutoka katika kitabu fulani cha Rüdder Köpper Verlag ambayo iliwaruhusu kuichapisha katika mkusanyo wetu.
Kitabu chetu kilitoka kwa kishindo kikubwa huko Kenya mwaka 2007. Kiliwavutia wasomaji wengi. Kutokana na mvuto huo, mwezi wa Disemba mwaka uliopita 2011, kitabu kiliteuliwa kuwa teule (set book) kwa mtihani wa taifa wa fasihi ya Kiswahili kuingia vyuovikuu vya Kenya. Hili ni jambo kubwa katika ufanisi wa kazi yetu, kwa sababu ni ushindani mkubwa kwetu na watoa vitabu wao.

Unaniuliza kwa nini kitabu chenye sifa hizi hakipatikani Tanzania? Kwanza, nadhani kwamba suala la utamaduni, hasa utamaduni wa maana halishughulikiwi katika nchi yetu. Yanayoshughulikiwa zaidi ni maslahi ya pesa na utajiri mkubwa. Inashangaza leo kwamba inakuwa vigumu kwa nchi zetu za Afrika Mashariki kuungana kiuchumi kwa maslahi ya watu wetu, lakini ni rahisi kushirikiana na madola makubwa ya dunia ambayo tunajua hayajali masalahi yetu.

 Jambo hili linasababisha ugumu wa vitu vidogo kama vitabu vya Kenya kuletwa Tanzania na vya Tanzania kupelekwa Kenya. Pili nchi yetu haina utamaduni wa usomaji vitabu na kwa hivyo watoa vitabu wa Kenya na Tanzania wanasitasita wakati kutoa vitabu vya aina fulani. Labda uandishi wa kitabu hiki unaweza kuonekana ni mgumu bila sababu yenye ukweli hasa. Tatu wananchi walio wengi Tanzania hawana kipato cha kutosha kununua vitabu badala ya kununua mkate wa kulisha watoto wao.
Profesa Said Ahmed Mohammed anayetukuza fasihi ya Kiswahili ndani na nje ya Afrika, alizaliwa mwaka 1947, Zanzibar.

2. Wewe Profesa na mwandishi maarufu wa Kenya Ken Walibora mmejitolea muhanga kutoa mkusanyiko huu mzuri sana unaounganisha pia waandishi wazuri muhimu wa Kiswahili mathalan marehemu Muhammed Said Abdullah ambaye baada ya kufariki 1991 ni kama hakusikika tena. Mmelifufua jina lake. Waandishi wetu muhimu hawathaminiwi tena siku hizi.

MAJIBU: Ni kweli kwamba waandishi na wasanii hawathaminiwi sana. Wanaothaminiwa nchini mwetu ni wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Mwanasiasa hata akiwa mdogo kabisa kama sheha au mjumbe wa nyumba kumikumi huweza kutukuzwa vikubwa sana kulingana na mwandishi aliye hai au aliyekufa. Hapa sisemi kwamba wanasiasa au wafanyabiashara wasithaminiwe, la! Kile ninachosema ni, ili taifa lipate watetezi wake, inahitaji kuthaminiwa kila mtu anayelilitumikia kwa njia moja au nyingine. Mimi ninayeishi nje ya Tanzania, naona jinsi ya jamii hizi za Ulaya zinavyojitahidi kumthamini na hata kumtukuza kila mwananchi ambaye anatoa mchango wake katika kuliendeleza mbele taifa lake. Kwa sababu hii, kuwekwa hadithi ya “Mke Wangu” ya Muhammed Said Abdulla katika kitabu chetu, kutasaidia wananchi wa Kenya na Tanzania kumkumbuka mwandishi huyu maarufu, kwani nani mwengine angemthamini na kumtukuza mwandishi ambaye alikuwa balozi wa Tanzania kupitia fasihi ya Kiswahili? Inasikitisha kwamba wakati mwingine Muhammed Said Abdulla anatukuzwa nje kuliko kwao Tanzania.

3. Utangulizi wa “Damu Nyeusi” unaongelea juu ya fani ya hadithi fupi fupi ambayo haithaminiki sana katika uchapishaji wa Kiswahili. Unaitathmini, kuieleza kinadharia na kuitetetea.

Wewe na Ken Walibora, wahariri wake, mnasema : “ Mustakabali wa hadithi fupi ya Kiswahili unaonyesha matumaini mazuri….Ni matumaini yetu kwamba wasomaji na wahakiki wa Kiswahili watadhihirisha utambuzi wao vile vile katika kudurusu hadithi hizi na nyinginezo zilizoandikwa zamani,zinazoibuka sasa na zitakazoibuka baadaye.”
Je mnaiona kazi makini mlioifanya kama mchango wa kuendeleza hatima ya hadithi fupi?
MAJIBU: Naam, ni kweli kabisa kwamba tulilenga kwamba kitabu hiki kiwe ni mfano mmojawapo wa hadithi fupi nzuri utakaokumbukwa kwa muda mrefu. Na naona tumefanikiwa. Hatuna shaka kwamba mchango huu wa hadithi hizi umewachangamsha na kuwachochea vijana wengi wa Kenya kujaribu kuandika. Kwa mfano, katika mkusanyo mwingine wetu ambao tumeuhariri mimi na Ken, unaoitwa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (Longhorn/Sasa Sema Nairobi), pia unakusanya hadithi za vijana wapya ambao wanajitambulisha na sisi katika kazi zao ambazo zinavutia sana.
Jambo hili linatufurahisha na kutupa fahari kubwa.Said Ahmed Mohammed keshatoa zaidi ya vitabu  30 – Riwaya 11 (ikiwepo” Asali Chungu” kigongo chake cha kwanza kilichomwagika uwanjani mwaka 1976), Tamthiliya 7, mikusanyiko minne ya Ushairi na mikusanyiko Saba ya Hadithi fupi ambayo moja wapo ni “Kiti cha Moyoni” alichochangia na Ken Walibora na “Damu Nyeusi” (pia  na Ken Walibora) kikatoka 2007. Mbali na vitabu, Profesa Said ambaye ni mhadhiri wa lugha za Kiafrika chuo kikuu cha Bayreuth, Ujerumani(toka 1997) na keshachapa vitabu vingi vya watoto wa shule za msingi ambavyo lengo lake kufundisha, kutukuza na kujenga lugha na fasihi ya Kiswahili.
Baadhi ya vitabu vyake Profesa Said Ahmed Mohammed – vyote vimechapishwa Kenya.

1. Mkusanyiko mzuri wa hadithi fupi za Kiswahili uliotolewa mwaka 2007 na Macmillan Kenya Publishers Nairobi. Inakuaje kitabu hiki chenye waandishi kem kem wakiwemo magwiji maarufu Chinua Achebe (Nigeria), Ama Ata Aidoo (Ghana) hakipatikani, hakijulikani wala kuongelewa, Tanzania?

MAJIBU:
Mkusanyo wa hadithi fupi Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine ni mkusanyo uliotayarishwa kutokana na pande mbili. Kwanza wazo na pendekezo lilikuja kwetu kutokana na kampuni ya Macmillan Kenya kwa wakati ule, yaani kabla Macmillan haijanunuliwa na kampuni ya Moron ambayo ndiyo inayomiliki

kitabu hiki sasa. Pili kampuni ya Macmillan ilimteua Ken Walibora na mimi tuwe wahariri wa kitabu kinachotazamiwa. Uteuzi huo ulipitia kwa meneja wa uchapishaji wao, Bwana John Mwazemba ambaye aliyekuwa mwenye hamu na mapenzi makubwa wa Kiswahili na fasihi yake na pia mweledi na mkakamavu katika kazi zake kwa jumla.

Ken na mimi tulikubali ombi la Macmillan kwa shuruti kwamba, tupewe uhuru wa kuchagua waandishi wa hadithi fupi zinazotakiwa. Tulilazimisha jambo hilo kwa madhumuni ya kuwatoa kumbini vijana chipukizi ambao wameshaonyesha dalili za uandishi mzuri. Hatukutaka kuchagua waandishi kwa misingi ya mlango wa nyuma. Masharti yetu yalikubaliwa na Macmillan. Tulichagua waandishi chipukizi ambao tulijua wana uwezo wa kuandika hadithi fupi nzuri. Kamwe hatukutaka kuchagua waandishi wa hadithi fupi kwa vigezo vya jinsia, ukabila, udugu, urafiki au uwananchi. Waandishi tuliowachagua ni Robert Oduori na Omar Babu kutoka Kenya na Mohamed Khelef Ghassany, Farouk Topan na Ali Abdulla Ali kutoka Tanzania.
Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe. Hadithi zilizochaguliwa ni Tropical Fish (Samaki wa Nchi za Joto) iliyoandikwa na Doreen Baingana kutoka Uganda, The Madman (Kichaa) iliyoandikwa na Chinua Achebe kutoka Naijeria, na In the Cutting of a Drink (Katika Kutiliwa Kinwaji) iliyoandikwa na Ama Ata Aidoo kutoka Ghana. Hadithi ya Muhammed Said Abdulla” Mke Wangu” ambayo ni hadithi ya zamani sana iliazimwa kutoka katika kitabu fulani cha Rüdder Köpper Verlag ambayo iliwaruhusu kuichapisha katika mkusanyo wetu.
Moja ya vitabu vya zamani vya mwandishi Mohammed Said Abdullah vyenye mhusika kachero mwerevu, Bwa’ Musa vilitumika mashuleni Tanzania. “Damu Nyeusi” imechangia kufufua jina la mzee huyu mashuhuri aliyefariki mwaka 1991, bila kishindo chochote.

Kitabu chetu kilitoka kwa kishindo kikubwa huko Kenya mwaka 2007. Kiliwavutia wasomaji wengi. Kutokana na mvuto huo, mwezi wa Disemba mwaka uliopita 2011, kitabu kiliteuliwa kuwa teule (set book) kwa mtihani wa taifa wa fasihi ya Kiswahili kuingia vyuovikuu vya Kenya. Hili ni jambo kubwa katika ufanisi wa kazi yetu, kwa sababu ni ushindani mkubwa kwetu na watoa vitabu wao.

Unaniuliza kwa nini kitabu chenye sifa hizi hakipatikani Tanzania? Kwanza, nadhani kwamba suala la utamaduni, hasa utamaduni wa maana halishughulikiwi katika nchi yetu. Yanayoshughulikiwa zaidi ni maslahi ya pesa na utajiri mkubwa. Inashangaza leo kwamba inakuwa vigumu kwa nchi zetu za Afrika Mashariki kuungana kiuchumi kwa maslahi ya watu wetu, lakini ni rahisi kushirikiana na madola makubwa ya dunia ambayo tunajua hayajali masalahi yetu. Jambo hili linasababisha ugumu wa vitu vidogo kama vitabu vya Kenya kuletwa Tanzania na vya Tanzania kupelekwa Kenya. Pili nchi yetu haina utamaduni wa usomaji vitabu na kwa hivyo watoa vitabu wa Kenya na Tanzania wanasitasita wakati kutoa vitabu vya aina fulani. Labda uandishi wa kitabu hiki unaweza kuonekana ni mgumu bila sababu yenye ukweli hasa. Tatu wananchi walio wengi Tanzania hawana kipato cha kutosha kununua vitabu badala ya kununua mkate wa kulisha watoto wao.
Profesa Said Ahmed Mohammed anayetukuza fasihi ya Kiswahili ndani na nje ya Afrika, alizaliwa mwaka 1947, Zanzibar.
2. Wewe Profesa na mwandishi maarufu wa Kenya Ken Walibora mmejitolea muhanga kutoa mkusanyiko huu mzuri sana unaounganisha pia waandishi wazuri muhimu wa Kiswahili mathalan marehemu Muhammed Said Abdullah ambaye baada ya kufariki 1991 ni kama hakusikika tena. Mmelifufua jina lake. Waandishi wetu muhimu hawathaminiwi tena siku hizi.

MAJIBU: Ni kweli kwamba waandishi na wasanii hawathaminiwi sana. Wanaothaminiwa nchini mwetu ni wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Mwanasiasa hata akiwa mdogo kabisa kama sheha au mjumbe wa nyumba kumikumi huweza kutukuzwa vikubwa sana kulingana na mwandishi aliye hai au aliyekufa. Hapa sisemi kwamba wanasiasa au wafanyabiashara wasithaminiwe, la! Kile ninachosema ni, ili taifa lipate watetezi wake, inahitaji kuthaminiwa kila mtu anayelilitumikia kwa njia moja au nyingine. Mimi ninayeishi nje ya Tanzania, naona jinsi ya jamii hizi za Ulaya zinavyojitahidi kumthamini na hata kumtukuza kila mwananchi ambaye anatoa mchango wake katika kuliendeleza mbele taifa lake. Kwa sababu hii, kuwekwa hadithi ya “Mke Wangu” ya Muhammed Said Abdulla katika kitabu chetu, kutasaidia wananchi wa Kenya na Tanzania kumkumbuka mwandishi huyu maarufu, kwani nani mwengine angemthamini na kumtukuza mwandishi ambaye alikuwa balozi wa Tanzania kupitia fasihi ya Kiswahili? Inasikitisha kwamba wakati mwingine Muhammed Said Abdulla anatukuzwa nje kuliko kwao Tanzania.

3. Utangulizi wa “Damu Nyeusi” unaongelea juu ya fani ya hadithi fupi fupi ambayo haithaminiki sana katika uchapishaji wa Kiswahili. Unaitathmini, kuieleza kinadharia na kuitetetea.
Wewe na Ken Walibora, wahariri wake, mnasema : “ Mustakabali wa hadithi fupi ya Kiswahili unaonyesha matumaini mazuri….Ni matumaini yetu kwamba wasomaji na wahakiki wa Kiswahili watadhihirisha utambuzi wao vile vile katika kudurusu hadithi hizi na nyinginezo zilizoandikwa zamani,zinazoibuka sasa na zitakazoibuka baadaye.”
Je mnaiona kazi makini mlioifanya kama mchango wa kuendeleza hatima ya hadithi fupi?

MAJIBU: Naam, ni kweli kabisa kwamba tulilenga kwamba kitabu hiki kiwe ni mfano mmojawapo wa hadithi fupi nzuri utakaokumbukwa kwa muda mrefu. Na naona tumefanikiwa. Hatuna shaka kwamba mchango huu wa hadithi hizi umewachangamsha na kuwachochea vijana wengi wa Kenya kujaribu kuandika. Kwa mfano, katika mkusanyo mwingine wetu ambao tumeuhariri mimi na Ken, unaoitwa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (Longhorn/Sasa Sema Nairobi), pia unakusanya hadithi za vijana wapya ambao wanajitambulisha na sisi katika kazi zao ambazo zinavutia sana. Jambo hili linatufurahisha na kutupa fahari kubwa.

Malenga wa Mvita.
Shaaban Robert.

Adam Shafi

1 comments:

  1. Napendezwa sana na masimulizi yako...Ni kweli kwamba waandishi na wasanii hawathaminiwi sana. Wanaothaminiwa nchini mwetu ni wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Mwanasiasa hata akiwa mdogo kabisa kama sheha au mjumbe wa nyumba kumikumi huweza kutukuzwa vikubwa sana kulingana na mwandishi aliye hai au aliyekufa. Hapa sisemi kwamba wanasiasa au wafanyabiashara wasithaminiwe, la! Kile ninachosema ni, ili taifa lipate watetezi wake, inahitaji kuthaminiwa kila mtu anayelilitumikia kwa njia moja au nyingine. Mimi ninayeishi nje ya Tanzania, naona jinsi ya jamii hizi za Ulaya zinavyojitahidi kumthamini na hata kumtukuza kila mwananchi ambaye anatoa mchango wake katika kuliendeleza mbele taifa lake. Kwa sababu hii, kuwekwa hadithi ya “Mke Wangu” ya Muhammed Said Abdulla katika kitabu chetu, kutasaidia wananchi wa Kenya na Tanzania kumkumbuka mwandishi huyu maarufu, kwani nani mwengine angemthamini na kumtukuza mwandishi ambaye alikuwa balozi wa Tanzania kupitia fasihi ya Kiswahili? Inasikitisha kwamba wakati mwingine Muhammed Said Abdulla anatukuzwa nje kuliko kwao Tanzania.

    ReplyDelete