Menyu

Swahili Hub

Wanamziki

Rose Muhando
Mwanamuziki wa kike wa nyimbo za kiinjili.
Rose Muhando ambaye hujulikana pia kwa jina la Rose Muhando;amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania) ni msanii maarufu wa muziki wa injili katika lugha ya swahili katika kanda ya Afrika Mashariki.
Rose,ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu,ni mama wa watoto watatu. Mama huyu alidai kuwa akiwa na umri wa miaka tisa alipata maono ya Yesu Kristo akiwa amelazwa. Aliteseka kwa muda wa miaka mitatu,na baada ya hapo alipona na kubadili dini(kuongoka) na kuwa mkristo.
Alianza fani yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya inayoitwa Kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la kianglikana linaloitwa Chimuli mkoani Dodoma.
Mnamo tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2005, Rose Muhando alipata tuzo ya mtunzi boramuimbaji bora, na tuzo ya msanii mwenye albamu bora ya mwaka wakati wa tamasha la tuzo za kiinjili, 2004.
Mnamo mwezi wa kumi na mbili, 2005, alishiriki katika tamasha la kiinjili ili kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha Dar es salaam.
Baadhi ya albamu zake ni pamoja na:
1.Kitimutimu.
2.Uwe Macho, 2004.
3.Jipange Sawasawa, 2008.[1][2].
_______________________________________________________________________________________
Masaibu yake
Msanii nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando ‘anabeba’ mzigo wa lawama kufuatia kuwepo kwa mpasuko ndani ya ndoa ya Promota maarufu wa muziki huo nchini, Alex Msama na mtangazaji wa Kituo cha Redio cha WAPO FM, Laura Bonaventure, Risasi Mchanganyiko limesheheni data...

Chanzo cha habari hii kimepasha kuwa, ndoa hiyo ina ‘masiku kibao’ sasa ‘inapumulia mashine’ huku Rose akitajwa tajwa kuhusika na mgogoro wake.

Chanzo hicho kikaendelea kuweka ‘nje’ siri kuwa, chanzo cha kuwepo kwa ufa katika ndoa hiyo ni kufuatia mke wa Msama, Laura kuchezwa na machale kuhusu ukaribu kati ya mumewe na Rose Muhando kiasi cha kukosa amani kama siyo furaha.

Habari zinazidi kumwagika kwamba, hali hiyo ikashamiri, ikanawiri, ikafika mahali hisia za mwanamke huyo zikawa wazi na hivyo kuanza ‘kumsomea’ mashitaka mumewe akitaka maelezo kuhusu ukaribu huo.
Habari zaidi zinapasha kuwa, licha ya kujitetea bila ‘mwanasheria’, bado mke huyo akaweka ngumu kuelewa hali iliyosababisha kila mtu kuanza kuishi kivyake ndani ya nyumba.

“Hii hali ilifika mahali kila mmoja akawa kivyake ndani, Msama akashika hamsini zake, mkewe naye anakumbatia zilizobaki,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Kubwa kuliko zote, kuna wakati Msama akipiga wimbo wowote wa Rose (Muhando), mkewe anazima redio au anapunguza sauti, moyo unamtuma kuwa, hisia zake zina ukweli.”

Habari zaidi zinasambaa kuwa, hata pale Msama anapokwenda Dodoma kwa shughuli za kikazi, mkewe hudhani ‘mista’ wake yupo ‘andapromisi’ na Rose hali ambayo imekuwa ikizidi kuvuruga ndoa hiyo.
Mambo yalipozidi kuwa mabaya, nyeti zinapasha, mke aliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda ‘kujichimbia’ sehemu moja jijini Dar es Salaam (Risasi linahifadhi jina kwa sasa).

UTETEZI WA WADAIWA
Kufuatia madai haya, Mwandishi Wetu alipiga ‘jaramba’ mpaka ofisini kwa Msama, Msama Promotion, Block 41, Kinondoni jijini Dar na kufanikiwa kuongea naye kwa kumpa ‘a e i o u’ ya ishu yake ambapo alipagawa kwa kuanza kutaka kujua ‘sosi’ wetu.

Alipokataliwa kutunza maadili, alisema mambo ya kifamilia yaachwe kwa wanafamilia, kwani ni jukumu lao kuweka sawa kwenye ‘korogesheni’ endapo mambo yataharibika.
“Mambo ya kifamilia yabaki kuwa hivyo, kama kuna tatizo linalomshirikisha Rose Muhando si kihivyo, hata wewe mkeo anaweza kukuuliza kuhusu mwanamke f’lani ukamwelewesha, akaelewa na mkaendelea na safari yenu ya maisha,” alisema Msama.

Risasi: Kwa hiyo ni kweli?
Msama: Nimeshakupa jibu kaka, mimi kwangu ni amani tu, hakuna wasiwasi wowote ule.
Aidha, Risasi likachanganya miguu kumsaka Laura, mke wa Msama lakini baadaye akapatika kwa njia ya simu ya kiganjani.

Kwa upande wake baada ya kupigwa ‘mashuti’ na Risasi alisema nyumbani kwake hakuna tatizo na wala hana kinyongo na Rose kisha papo hapo akamwomba Mwandishi amtwangie simu baada ya dakika tano, (eti) ana mgeni.
Mwandishi alizifuata sekunde kwa macho angavu hadi zilipotimu dakika tano, alipopigiwa tena, cha ajabu, akawa anakata simu.

Risasi halikuchoka, likamgeukia bingwa wa muziki wa Kwaito, Rose Muhando ambaye kwa ‘binafsi’ yake alisema tuhuma dhidi yake na Alex Msama ni maneno ya ‘wachovu’ wa kiimani, lakini akakiri kuwa karibu sana na Promota huyo kwa sababu za kikazi.

Alipobanwa kuhusu madai ya malalamiko ya Laura, Rose alisema anaapa kwa Mungu wake hakuna ‘malavidavi’ kati yake na Msama na Laura kwake ni wifi yake kwa kuwa Msama kwake ni kama kaka yake ingawa si wa damu moja.

KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mwaka 2007, gazeti moja (siyo la Global) liliwahi kuripoti kuwepo kwa uhusiano usiofaa kati ya Msama na Rose, wakati huo Promota huyo alikuwa kwenye vikao vya maandilizi ya harusi yake na Laura, lakini wenyewe waliruka ‘kimanga’.

0 comments:

Post a Comment