Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

MWANDISHI ADAM SHAFI


MWANDISHI ADAM SHAFI

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…

Shaaban Robert


Maisha
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti. Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.

Lugha ni Njia


UTANGULIZI
Lugha imewahi kufafanuliwa kwa jumla kama mfumo wa sauti za nasibu za kusemwa zinazotumiwa na watu wa jamii Fulani wenye utamaduni unaofanana kwa madhumuni ya mawasiliano katika jamii hiyo.
Wataalamu wengi wa isimu (sayansi ya kuchanganua lugha na kuieleza jamii) kamusi ya kiswahili sanifu TUKI 1981 oxford press uk. 86 na lugha wanaelekea kukubaliana kwamba lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumini ya mawasiliano kati yao ( massam ba D.P.B na wenzake 1999, TUKI).