Menyu

Swahili Hub

Jifunze Fasihi


Fasihi kama dhana, imeelezwa na wengi kwa kuegemea nadharia na mitizamo
mbali mbali.  Hata hivyo ni muhimu tufahamu ya kwamba maana inayopewa dhana au
kitu fulani, huwa inachukuana na matumizi ya dhana yenyewe, watu wanaohusika,
mahali dhana hiyo inamotokea, na hata kipindi au wakati husika.  Hii ndiyo sababu
twapata maana mbalimbali zikitolewa kuhusu fasihi.  Kwa mfano, waandishi wengi wa
Kimagharibi wamesisitiza kwamba fasihi yahusu tu kazi zilizoandikwa.

Katika usomi wa kimagharibi, fasihi humaanisha maandishi ya wakati au nchi
fulani, hasa ile yenye kupewa thamani ya juu katika mtindo na uendelezaji wake.
Ufafanuzi huu unaotilia mkazo uandishi walenga kueleza kwamba fasihi ni amali
ya jamii zilizovumbua sanaa ya uandishi.[tafsiri yangu]

Kwa hivyo, fasihi, kulingana na mtizamo huo wa kimagharibi, imechukuana na uandishi,
na hivyo basi fasihi si fasihi mpaka iandikwe.  Bila shaka mtizamo kama huu hupuuza
fasihi-simulizi.  Ama kwa hakika hiyo hatua ya kuihusisha fasihi na maandishi ni ya

Add caption
maksuudi inayodhamiriwa kuonyesha fasihi kama amali ya jamii yenye taluma ya kusoma na kuandika.  Ni kile kitendo cha kibinafsi au cha kubagua ambacho hudhamiria kuonyesha jamii ambazo hazina taaluma ya uandishi kama jamii duni. Ukweli ni kwamba pamewahi kuwepo na bado zipo kazi za fasihi  kutoka kwa jamii ambazo hazikuwa na taaluma ya kusoma na kuandika.  Isitoshe, pana
mifano kemkem ya kazi zilizokuwa katika masimulizi hapo awali, lakini sasa zimehifadhika katika maandishi na huratibiwa kama kazi za fasihi.  Kazi nyingi za ushairi
7wa Kiswahili ni mifano ya kazi kama hizo.

Tunashurutika kukataa ufafanuzi huu unaotenga na kubagua; na badala
yake kuunda ufafanuzi wa kimapinduzi utakaoionyesha fasihi kama
inayochukua kazi zote za kubuniwa za wanadamu zinazoelezwa kwa
maneno. [tafsiri yangu]

Mtizamo kama huu waitizama fasihi kama kazi inayoendelezwa kwa maneno, iwe
andishi au simulizi [kuandika na kusimulia ni mtambo tu wa kuiwasilisha kazi hiyo].
Kuandika sawa na kuchonga au kuchora ni njia ya kueleza dhana tu, na jinsi ambavyo
mchoraji hutumia rangi katika kazi yake, mtunzi wa kazi ya fasihi hutumia maneno
kueleza dhana na hisia zake.  Maneno hayo huenda akayaandika, akayaimba au
akayazungumza.  Kwa hivyo, fasihi iwe imeandikwa au imesimuliwa bado ni fasihi.
8Naye Odaga (1985:xxi) anasema kwamba;
  Fasihi ni sanaa ambayo mtambo wake ni neno na
kiini chake ni binadamu. (Tafsiri yangu)
P’Bitek (kama hapo juu) anasema;
Fasihi husimamia kazi zote bunifu anazozitumia
mwanadamu kujieleza kwa maneno ambayo yaweza kuimbwa,
kusemwa, au kuandikwa.

  iliyo zaidi ya lugha.  Ni dhana na hisia
zilizovingikwa katika muziki wa lugha.
Na huchukua umbo la maneno na picha
zilizowekwa pamoja na ubunifu.  Fasihi
ni jinsi ya kuona, kuhisi, kufahamu.
 
Kwa muhtasari twaweza kusema kwamba pana kauli hizi za kimsingi ambazo hujitokeza
katika fafanuzi za wataalam hawa na wengine wengi kuhusu dhana ya fasihi:
 - Fasihi ni sanaa inayodhihiri ubunifu
 - inayotumia maneno kuwasilisha mambo yake
  - na ambayo hulenga binadamu kama kiini chake n.k.

Kama tulivyotaja hapo awali maana ya neno au dhana yoyote hutegemea mambo
mengi na hivyo basi fasili hii yetu ya fasihi huenda isichukuane na maoni ya mwingine
anayechagua kuitazama fasihi kwa njia tofauti.  Lakini hata mhakiki atumie mtizamo
gani, fasili yake pamoja na hitimisho lake litategemea anachukua fasihi kumaanisha nini
9pamoja na jukumu la mtunzi wa fasihi hiyo.  Katika misingi hii, huenda likawa jambo
mwafaka kuzingatia baadhi ya vigezo vilivyowahi kutumiwa katika kufafanua fasihi ili
Add caption
tupate msingi wa kufanya uhakiki.

 Pametokea vigezo tofauti vya kuifafanua fasihi kutegemea msisitizo anaotaka
kuweka mfasili pamoja na maendeleo na mabadiliko ya maisha kihistoria.  Kuna wale
wanaosisitiza umbo la nje la fasihi ambao wamekita nadharia zao katika muundo huo
ilhali wengine wanasisitiza umbo lake la ndani.  Pana wale wanaochagua kuzingatia
wahusika katika kutungwa kwa kazi hiyo, yaani mtunzi, hadhira yake na hata athari za
jamii.  Ndiposa twapata vigezo vilivyotumiwa ama vyalenga maumbo ya fasihi, maudhui
yake au yote mawili.

Ni muhimu kueleza kwamba hivi vigezo tutakavyovitaja hapa, mara nyingi
vimejitokeza katika utanzu wa uhakiki, hivi kwamba maelezo ya 'fasihi ni nini'
yanatumiwa kutathimini kutimizika kwa masharti yanayozingatiwa na mtunzi anapotunga
kazi yake.  Kwa hivyo kama utunzi wa fasihi husisitiza maudhui mbali mbali basi huenda
mhakiki akatumia kigezo hicho hicho katika kazi yake ya uhakiki kubainisha kufaulu
kwa kazi hiyo katika lengo hilo.

Hapo baadaye tutaangalia baadhi ya vigezo vinayotumiwa katika kuifafanua fasihi...

0 comments:

Post a Comment