Julius Nyerere, President of Tanzania, during a meeting with US president Jimmy Carter, August 4th, 1977. (Photo credit: Wikipedia) |
Mradi mkubwa kuunganisha wazungumzaji wa Kiswahili Afrika Mashariki umeanzishwa na magazeti ya Mwananchi na Taifa Leo, Kenya.
Ingawa ukiongea na wananchi nyanda mbalimbali Afrika Mashariki na Kati watasema Watanzania “mnaongea Kiswahili kikali”, ” cha moto”, “kizuri, “cha nguvu”, nk – sidhani kama kiutaratibu tunakithamini na kukijenga kama miaka 30 au 40 iliyopita enzi za Mwalimu Nyerere.
Kinachozidi kuharibu ni hili suala la Kiswanglish- ambacho hakieleweki kuku, mwiba, gari, kidevu, au jiwe-(ah tuyaaache hayo).
Hivyo hizi ni habari nzuri sana kuendeleza lugha hii kubwa duniani.
Angalia tovuti la -SWAHILI HUB- inayojumuisha waandishi sehemu zote za Afrika Mashariki- kujiunga pamoja kudumisha Kiswahili:
0 comments:
Post a Comment