Menyu

Swahili Hub

Pastor Michael Njoroge na Kahaba



Ama kweli siku za kiama zinukiapo, dalili wazo hudhihirika. Mambo yanayotukia siku hizi hata mfano mwafaka hamna. Ajabu iliyoje kumwona kasisi Michael Njoroge akiwatumia mahawara ili kukudhi mahitaji yake binafsi?


Nilipokuwa kwenye uchanga wangu, niliwatazama makasisi wa nyakati hizo kwa jicho pevu na lengo lao katika uwanda wa injili. Niliyashuhudia mengi na kwa hakika, tabia na nyendo zao zilikuwa waa. Lakini siku hizi, "Ibada ya kanisani imegeuzwa biashara. Hayo yamebainika katika kanisa moja la Embakasi hapa jijini Nairobi, ambapo mhubiri mmoja amejitafutia umaarufu kwa njia za ulaghai. Mhubiri amekuwa akishirikiana na makahaba kuwalaghai waumini." [Mohamed Ali] 

Sijuwi Palipokwenda Mrama!



Labda ni ile tamaa ya utajiri wa fumba fumbua na kule kupenda kuwa maarufu ala kulihali. Na hilo lina madhara ambayo aidha huchukua muda kabla ya kuyatambua au kabla ya wayo kufukuliwa... Si vyema binadamu kuzidi kuwatia wengine dhalamani ilhali anafahamu fika kuwa hiyo ndo Sirati. Hakika sisi hupumbazwa, na wakumlaumu hamna maana'ke binadamu ni yule yule, afikapo pahala na kiwango cha kumwamini insi mwenzake, huwa ameyaona mengi [Ya shari na heri]. Hapo, hufanya uamuzi kuzifuata nyayo za mwumba wake ili angaa utulivu umvae.

Mambo hukorogeka anapogundua chui binadamu si binadamu hata chembe, bali chui mla watu na ambaye aghalabu hugeuka na kuwa fisi; tena mlafi zaidi!

Natamani Dunia ifike ukomo iwezekanavyo kabla hatujawaona makasisi wengine kama Pastor Michael Njoroge wakichimbuliwa kwa zao israri.. Poster Michael ni mwiba katika jamii na ambao amewanyima imani wananchi wengi. Si ajabu jumapili ikawa siku sawia na siku zingine za juma sasa; Mbona mtu aende kanisani na huko viongozi hamna? Vichwa vimeoza- mfano wa samaki aozavyo kichwani kisha mwili mzima huambukizwa. (Na pana tofouti gani ya viongozi wetu na sisi wananchi?)

Tafakari!!!

(Utapeli Kwa Jina la Mungu)

2 comments:

  1. Sijui niseme nini! sasa wizi wa mabafu ni kanisani, mabomu yanatupwa kanisani na hata uhawara umeingia kanisani. tufanye nini? fauka ya haya kanisa si jumba bali ni mioyo ya binadamu! ningali na kanisa langu!!!!!smart simat

    ReplyDelete
  2. Bwana Paul, Ama kwa hakika, dunia gunia. Dunia na watu wake huhadaa na kughilibu... Dunia ni bahari iliyojaa papa na papaupanga ambao ukiwapapia kwa pupa na papara, hutokosa kupapatika kwa majuto makuu. Akili kichwani!!!

    ReplyDelete