Malenga wa Mvita Ahmad Nassir
AHMAD NASSIR ni mzee
mswahili wa Mombasa. Kwa upande wa babake ni Mtangana na kwa mamake ni
Mkilindini. Hizi ni miongoni mwa kabila za asili ya Kiswahili za ki-mvita,
yaani MombasaBwana Ahmad alizaliwa kuze, Mombasa mnamo 1936. Kama watoto
wengine wa kimombasa wa wakati huo aliingia chuoni kusoma kuraani na dini ya
kiislamu. Mafunzo hayo aliyapata kwa babu yake Sheikh Muhammad Ahmad Matano,
mpaka alipohitimu.
PENDO LA SIRI. [23/05/2012]
PENDO LA SIRI.
[23/05/2012]
Hayo ya hayawi hayawi, yaliniangukia kama nanga. Kiza kilichojimwaya kati ya upenyu wa mwanga katika aushi yangu. Yapo niliyoyaamini; Anenae kuwa pendo, si faida ni uvundo. Huyo yu katika mwendo, wa ujinga na ubaya. Na'mi kwa ari ambayo sikufahamu mwanzo wake, nikatii amri yakuwa tupendaneni, tusitendeyane ubaya...
Ama kwa hakika yalianza kama mchezo. Mara 'My son', mara wavutia mara sijui nini:- almuradi niliungulika na mengine kuyatia asali bandia. Nikajitia upofu kwa dhana kuwa mapenzi ya mtandaoni
Jifunze Fasihi
Fasihi kama dhana, imeelezwa na wengi kwa kuegemea nadharia na mitizamo
mbali mbali. Hata hivyo ni muhimu tufahamu ya kwamba maana inayopewa dhana au
kitu fulani, huwa inachukuana na matumizi ya dhana yenyewe, watu wanaohusika,
mahali dhana hiyo inamotokea, na hata kipindi au wakati husika. Hii ndiyo sababu
twapata maana mbalimbali zikitolewa kuhusu fasihi. Kwa mfano, waandishi wengi wa
Kimagharibi wamesisitiza kwamba fasihi yahusu tu kazi zilizoandikwa.
Lugha Tukufu ya Kiswahili
Historia ya Kiswahili
Maeneo penye wasemaji wa Kiswahili
Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.
Neno Swahili ni neno la asili ya Kiarabu Sahil lenye maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ (السواحلي) ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani.
Yaliyomo [ficha]
1 Mwanzo katika miji ya pwani
2 Lugha ya biashara
3 Kiswahili wakati wa ukoloni
4 Kiswahili leo
Lugha ni?
Wanamziki
Mwanamuziki wa kike wa nyimbo za kiinjili.
Rose Muhando ambaye hujulikana pia kwa jina la Rose Muhando;amezaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania) ni msanii maarufu wa muziki wa injili katika lugha ya swahili katika kanda ya Afrika Mashariki.
Waandishi Mashuhuri wa Vitabu
Said Ahmed Mohammed
Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe. Hadithi zilizochaguliwa ni Tropical Fish (Samaki wa Nchi za Joto) iliyoandikwa na Doreen Baingana kutoka Uganda, The Madman (Kichaa) iliyoandikwa na Chinua Achebe kutoka Naijeria, na In the Cutting of a Drink (Katika Kutiliwa Kinwaji) iliyoandikwa na Ama Ata Aidoo kutoka Ghana. Hadithi ya Muhammed Said Abdulla” Mke Wangu” ambayo ni hadithi ya zamani sana iliazimwa kutoka katika kitabu fulani cha Rüdder Köpper Verlag ambayo iliwaruhusu kuichapisha katika mkusanyo wetu.
Hadithi
Wosia Wa Babu
Furaha iliyo’je kuwa kwenye kigonda changu wakati kama huu wa magharibi?. Ha! Ha! Ha!... Siniulize mbona nimekenua ‘ivo, ipo siku katika umri huu wangu, utaijua sababu. Eti watamani kujua sasa ‘ivi?, aha! basi ni hivi, wapo wenye imani kuwa kuishi ni lazima almuradi keshazaliwa. Kubugia chumvi si sheria. Ni kwa kudura zake tu Rabana. Kupata dakika ‘izi za kusema nanyi wajukuu wangu, si kwa umri wangu, si kwa uwezo wangu, si kwa utajiri wala uchochole wangu. Ni majaliwa yake Jalali!.http://visauswahilini.wordpress.com/2012/02/20/kisa-changu/
Pendo la siri.
Pendo la siri.
Makala
Yuko ambaye hajui na hajui kuwa hajui. Huyu ni banadamu ambaye kwake hakuna anachokijua hata kidogo, lakini siyo kwa kosa lake ila bado hajajuzwa juu ya mambo. Kwa jina la karibu twaweza kumwita Mjinga. Ujinga siyo tusi ila tafsiri yake ni mtu yeyote ambaye hafahamu wala hajui chochote. Kwa mfano, wewe kama hujui kitu chochote basi ni mjinga na ukumbuke kuwa ujinga siyo tusi. Lakini pamoja na hayo yote, binadamu wa sampuli hii, huwa hasemi asiyoyajua. Mintaarafu, ukikutana na binadamu wa namna hii ujue kuwa ni mjinga na anahitaji msaada ili kuyajua mambo. Mjinga!!!











