Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

Mama Kanumba Alazwa!!


MAMA mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa juzi alilazwa katika Zahanati ya Kilimani, Manzese jijini Dar kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu pamoja na Malaria.

Machangu Waona cha Mtemakuni!


Machangu wamekiona cha mtemakuni! Wakati Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukiwa katika chungu cha nane, akina dada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili maarufu kama Machangudoa au Chipsi Funga au Wauza Sukari Tamu, wamekula viboko laivu baada ya kutuhumiwa kuwatega Waislamu.

Keitta, Alex wamtabiria Lady May ushindi


Baada ya kutolewa kwa washiriki, Keitta wa Ghana na Alex wa Kenya, wote wamemtaja mshiriki kutoka Namibia, Lady May kuwa anaweza kuibuka mshindi.

Kinara wa Hollywood anayeongoza kwa kipato- Tom Cruise


MCHEZA Filamu Thomas Cruise Mapother maaarufu kama Tom Cruise  ametajwa kuwa miogoni mwa waigizaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha nchini Marekani.

Gharama zimezidi shule binafsi



NASHUKURU kwa kupata nafasi katika gazeti lako leo, lakini zaidi hasa nakupongeza kwa nzuri unayoifanya.


Mimi ni mzazi mwenye watoto wanaosoma shule za sekondari za  binafsi, ingawa walichaguliwa na Serikali lakini  nikaona niwapeleke  huko labda watapata elimu bora, lakini imekuwa kama wanatufanya sisi mitaji.

Hifadhi ya Mkomazi inayo mengi ya kujionea


NI takribani miaka mitatu tangu pori la akiba la Mkomazi libadilishwe na kuwa hifadhi ya taifa. Kipindi hiki si kirefu lakini yapo mengi ya kujivunia kwa hifadhi hii inayolitangaza taifa duniani kote.

Kigezo cha watu kusaliti katika mapenzi


UNAHISI mwenzi wako anakusaliti kwa maana kwamba anafanya ngono na wanawake au wanaume wengine? Fahamu kuwa wapo wengi wenye kulalamikia hilo.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini hasa anatoka na wengine ikiwa aliahidi kwamba atakuwa ananipenda milele? Wengine wanakwenda mbali zaidi na kufikiri kila kitu ambacho anakifanya kwa mwenzi wake kitakuwa ni chenye kumpendeza mwingine.
“Mimi najitahidi kumfanyia mambo mengi mazuri, bado anaonekana haridhiki,” ndivyo baadhi ya watu wanavyojisemea.

Uingereza, New Zealand kufungua Olimpiki


TIMU ya taifa ya wanawake ya soka ya Uingereza inatarajiwa kupata ushindi mkubwa katika mechi ya leo ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki dhidi ya New Zealand. Mechi hiyo inachezwa leo ikiwa ni siku mbili kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya Olimpiki ambayo ni michezo mikongwe duniani.

Mbinu za Lugha ya Kiswahili


Mbinu za Lugha
Katika fasihi, mwandishi au msimulizi anaweza kupitisha ujumbe wake kwa njia mbali mbali zinazomwezesha kuwasilisha ujumbe wake vizuri na kwa lugha inayopendeza. Kuna tanzu mbili za mbinu anazotumia mwandishi/msimulizi wa fasihi:
a) Mbinu/Fani za Lugha 
b) Mbinu za sanaa
Mbinu za lugha hutambulikana moja kwa moja kutokana na uteuzi wa maneno yaliyotumika. Msomaji hahitaji kusoma kifungu kizima ndipo mbinu hiyo ijitokeze.
Mbinu za sanaa humhitaji msomaji asome kifungu kizima, au hadithi yote ndipo mbinu iliyotumika ijitokeze.
{Mbinu za Lugha ya Kiswahili}