Menyu

Swahili Hub

Gharama zimezidi shule binafsi



NASHUKURU kwa kupata nafasi katika gazeti lako leo, lakini zaidi hasa nakupongeza kwa nzuri unayoifanya.


Mimi ni mzazi mwenye watoto wanaosoma shule za sekondari za  binafsi, ingawa walichaguliwa na Serikali lakini  nikaona niwapeleke  huko labda watapata elimu bora, lakini imekuwa kama wanatufanya sisi mitaji.



Kila kunapokucha watoto huja na barua kutoka shule ya mchango mara wa jingo mara maabara, mara masomo ya mwezi  na mambo mengine kadha wa kadha hadi unajikuta unakosa cha kuwapa kupeleka.


Lakini ukikagua madftari ya watoto hawafundishwi karibu kila siku na hata mitihani wanachelewa kurudishiwa, sasa unajiuliza  fedha wanazoomba kila siku hufanyiwa nini?


Jamani kwanza ningeomba shule hizi zipunguze karo, kwani ni kubwa lakini pia kama wanatoza wanafunzi  fedha za michango kila mara basi tuone juhudi zao kwa matokeo bora ya wanafunzi.


Kero hii ni ya muda mrefu ningeomba shule za binafsi zifundishe kadri wanavyotoza ada. 


<<<<<

0 comments:

Post a Comment