Menyu

Swahili Hub

Kinara wa Hollywood anayeongoza kwa kipato- Tom Cruise


MCHEZA Filamu Thomas Cruise Mapother maaarufu kama Tom Cruise  ametajwa kuwa miogoni mwa waigizaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha nchini Marekani.


Tom  Cruise ambaye pia ni muandaaji wa filamu amejizolea umaarufu kupitia filamu mbalimbali zikiwemo Top gun,Mission imposible,The last Samurai,Rock of ages,Knight and Day na nyinginezo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Fobres Tom Cruise analipwa dola milioni 75 sawa na pesa za kitanzania bilioni 120 akiwaacha mbali waigizaji wengine akiwemo Leornardo Dicaprio na Adam Sandler wanaolipwa dola milioni 37 kila mmoja.

Chanzo hicho cha habari kinafafanua kuwa Cruise amefikia mafanikio hayo ya mwakia baada ya kufanya vizuri kwa filamu yake ya Mission Impossible - Ghost Protocol aliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana ambayo ilingiza dola milioni  700.

Pamoja na  kushika rekodi hiyo  Cruise anakabiliwa na misukosuko ya familia hali iliyosababisha hivi karibuni  kutengana na mkewe Katie Holmes aliyedumu naye takribani miaka  mitano aliyebahatika kupata naye mtoto mmoja aitwaye Suri  Cruise.

Taarifa zilizosambaa katika mitandao zinabainisha Katie amefikia maamuzi hayo kama njia ya kujiweka mbali yeye pamoja na binti yake kujihusisha na imani ya Scientology ambayo Cruise amesimamia.

Maisha ya ndoa
Cruise ambaye ni muumini wa dhehebu la ‘Scientology’ anaripotiwa kufunga ndoa mara tatu ambapo imebainika kuwa Mimi Rogers ambaye alikuwa mke wake wa kwanza ndiye aliyemuingiza katika dhehebu hilo linalopinga awepo wa Mungu na kuamini sayansi .

Hata hivyo ndoa ilidumu kwa miaka mitatu tu kabla ya kutalikiana na kufunga ndoa tena  na muigizaji mwenzie Nicole Kidman ambapo walidumu kwa muda wa miaka 11,wawili hao walifanikiwa kuhasi watoto wawili Issabela na Connor Cruise.

Tuzo alizopata
Miongoni mwa tuzo alizowahi kujinyakulia mcheza filamu huyu ni pamoja na tuzo ya MTV kupitia filamu yake ya The Last Samurai iliyomuwezesha pia kupata tuzo ya AFI kama filamu bora ya mwaka 2003 nchini Marekani.

Cruise pia alifanikiwa kutwaa tuzo maalumu ya mchezaji bora wa filamu kwa mwaka 1987 huku mwaka 2002 akipata tuzo ya Muigizaji bora  kupitia filamu ya Vannila Sky  na tuzo nyingine nyingi ambazo amezipata mpaka hivi sasa.

Historia kwa ufupi
Alizaliwa July 3, 1962 katika mji wa New York nchini Marekani,alipofikisha miaka 14 alijiunga katika shulee ya seminari akiwa na lengo la kuwa padre lakini haliachana na ndoto hizo baada ya mwaka mmoja.

Akiwa na miaka 16 mwalimu wake alimshauri kushiriki katika muziki na alipajiribu alijigundua kipaji chake ndipo hapo alipoanza rasmi kucheza filamu.

<<<<

0 comments:

Post a Comment