Menyu

Kiswahili

Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa Kiafrika na Kiislamu ukajielewa kuwa sehemu ya dunia ya Uislamu.

SWAHILI HUB

BLOGU YA KISWAHILI KWA AJILI YA KUSAFISHA FIKRA ZA WAAFRIKA!

DUNIYA MTI MKAVU

Kiumbe siulemee kamwe... Likuondokealo, lina heri nawe.

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomok...

Said Ahmed Mohammed

Uamuzi wa kuchagua hadithi zilizoandikwa kwa Kiengereza kufasiriwa kwa Kiswahili, ulitokana na Macmillan wenyewe. Nao walizichagua hadithi hizo kwa ubora wa hadithi zenyewe na umaarufu wa waandishi wenyewe.

Swahili Hub

Ati, binadamu amegeuka na kuwa nguruwe?



wakati mwengine binadamu – yule kiumbe mwenye akili sana mpaka akajipachika cheo cha “U-Homo Sapiens” – anaweza kukushangaza na kukufanya uusaili ubinadamu wake. Na hapa sizungumzii vita au matatizo yake mengine anayojisababishia. Hebu soma kisa hiki kifupi.

Kuhusu uhuru wa dini


UTANGULIZI
1. Wanadamu wa nyakati hizi wanazidi kuwa macho sana kuhusu HESHIMA YA KIUTU (Dignitatis Humanae)[1]; na inaongezeka idadi ya wale wanaodai kuwa binadamu wafanye mashauri yao wenyewe na washike wajibu wao kwa uhuru katika vitendo vyao na wasiwe watendaji wa kulazimishwa, bali waongozwe na hisia ya wajibu wao. Wakati huohuo wanadai kikomo cha kisheria cha nguvu ya serikali ili kuzuia

Umuhimu Wa Maisha ya Binadamu




Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini


UTANGULIZI

Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili na kuiweka katika mizani, upande mmoja ubebe tahakiki zilizozingatia maudhui na mwingine zile zilizoangaza fani, upande wa maudhui utalemewa na uzito na kuanguka. Ni kweli kuwa umuhimu wa fasihi katika jamii unatokana na jinsi ambavyo inaimulika jamii na kuichora kwa madhumuni ya kuihakiki na 

Wanaume msiogope kutahiriwa


WASWAHILI husema kazi ni kazi! Wengine husema kazi nzuri ni ile iliyouwezesha mkono kwenda kinywani. Lakini, kwa bahati mbaya, baadhi ya wanajamii hasa wa siku hizi wamekuwa wakichagua kazi huku wengine zaidi vijana, wakidai kuwa hakuna ajira.

MWANZO MWEMA SIO MWISHO MWEMA


Magoma bi bi bi! ndiyo yalinigutusha kutoka usingizini. Mara nilisikia ile sauti nyororo kama kinanda ya ngoi ikiongoza wimbo, ambao kwa kawaida uliimbwa katika sherehe za arusi. Niligutuka kwa haraka, kuitupilia blanketi yangu mbali na kujisongeza dirishani na kupenyeza pazia. Kumbe kulikuwa kumekucha kwa kiasi hicho!

CHINI YA SHAMSHI

Mjomba'ngu Shamshi
Kuzaliwa kwangu kulifululizwa na majonzi yas’o kuwa na mfano. Hili si ada kwa wana wengi duniani. Na kama ilivyokuwa kawaida katika jamii za kwetu Raha, waliniona mwenye shari hivyo kunipa jina Tabu. Japo haya si kuyanga’mua papo kwa hapo, niliyafahamu mtuo kwa mtuo kadri miaka ilivyozidi kuporomoka.

MWANDISHI ADAM SHAFI


MWANDISHI ADAM SHAFI

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…

Shaaban Robert


Maisha
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 kijiji cha Vibambani jirani na Machui kilomita 10 kusini mwa mji wa Tanga, alipata elimu yake katika shule ya Msimbazi, jijini Dar-es-salaam kati ya miaka 1922 na 1926 alifaulu na kupata cheti. Akaajiriwa na serikali ya kikoloni akawa karani katika idara ya forodha huko Pangani mwaka 1926 – 1944. Bila shaka kukaa kwake miaka mingi hivi katika mji wa kihistoria uliokuwa mahali pa utamaduni wa Kiswahili tena mahali patulivu kumesaidia maendeleo yake Shaaban kama mwandishi wa Kiswahili.